Header Ads Widget

HABARI KATIKA PICHA: WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI DUNIANI



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia waandamanaji katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika  kitaifa kwenye  viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro, Disemba 1, 2023. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima na kulia ni Mwenyeki wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Afya na masuala ya UKIMWI, Stanslaus Nyongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 



Waandamaji wakipita mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika  Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja wa vya Shule ya Sekondari Morogoro, Disemba 1, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi alipowasili kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Shule ya Sekodari Morogoro, Disemba 1, 2023.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima na wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtalaamu wa Afya ya Jamii, Makune Makune (kushoto)  wakati alipotembelea banda la maonesho la Programu  ya  Marekani inayojishughulisha na masuala ya UKIMWI (PEPFAR) kabla ya kuhutubia katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI  Duniani  kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro, Disemba 1, 2023. Kulia ni Mratibu wa Programu hiyo, Jesca Green. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI