Header Ads Widget

CRDB NA ZHC WATIA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO


NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR BENKI ya CRDB imetiliana saini na Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC) ya kuwawezesha wateja wa makundi mbalimbali kumiliki Nyumba katika miradi inayosimamiwa na shirika hilo katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.Akizungumza mara baada ya kutiliana saini hiyo hafla ambayo ilifanyika katika Ofisi ya Benki ya CRDB Michenzani mall, Kaimu Mkuuwa Idfara ya wateja wa awali na wa kati wa Benki ya CRDB, Stehen Adili, alisema, makubaliano hayo yatakwenda kuwanufaisha wateja wa makundi mbalimbali kwa kupata mkopo wa thamani ya hadi shilingi Bilioni 1.Alisema, Makundi hayo ni pamoja na wafanyakazi wa mashirika au taasisi, wanachama wa Mifuko ya Penshen, wajasiriamali waliojiajiri katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) na watanzania waishio nje ya nchi wanaomiliki hati za kusafiria za nchi nyengine.
Aidha alisema kusainiwa kwa makubaliano hayo ni muendelezo wa jitihada za benki ya CRDB katika kuwawezesha watanzania kumiliki makazi bora ambapo kwa takwimu za TMRC hadi mwezi June 2023.Hata hivyo, alifahamisha kuwa Benki hiyo ndio kinara wa utoaji wa mikopo ya nyuma ambapo katika mikopo yenye tathmini ya Takribani Bilioni 593.76 iliyotolewa na taasisi za fedha ambapo benki yao imetoa takribani bilioni 197.70 sawa na asilimia 33.3.Hivyo, aliihakikishia ZHC kuwa wataendelea kufanya nao kazi na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuboresha hali ya makaazi Zanzibar, ambapo utekelezaji wa miradi chini ya uongozi wa awamu ya nane ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kukuza hali ya makazi ya wananchi wa Zanzibar.‘Benki nasi tunaungana nae katika jitihada hizi kwa kuhakikisha kuwa tunawawezesha wananchi wa Zanzibar na duniani kote kuweza kumiliki makazi bora kwa gharama nafuu’ alisema.Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHS), Mwanaisha Ali Said, alisema, makubaliano hayo yatawawezesha kukamilisha vyema nyumba hizo sambamba na kuipongeza benki ya CRDB kwa kuendeleza umoja huo.Aidha alisema fursa hiyo itawaongezea kufanya kazi katika miradi mipya inayotarajiwa kufanyika kupitia njia taslim, kulipa kwa awamu na njia ya mkopo ambapo alisema njia ya mkopo ilikuwa bado haijafanya vizuri, hivyo kufanyika makubaliano hayo shirika la nyumba litawasaidia kupata wateja katika njia ya tatu ya mkopo.Hivyo, alisema saini hiyo itagusa miradi yote inayotarajiwa kujenga baada ya Mombasa na wanampango kujenga maeneo ya Nyamanzi na kuwataka wannachi kupeleka maombi yao kwa kutumia nyumba za mfikiwa Pemba sambamba na kuahidi kuwa shirika linaendelea kutatua changamoto mbalimbali kwa ajili ya makazi ya nyumba iliyokuwa bora.Mapema, Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Zanzibar Abdalla Duchi, alisema Benki yao itaendelea kufanya kazi na serikali pamoja na taasisi mbalimbali ili kuona wananchi wanapata huduma za kimaendeleo kupitia benki hiyo.

Post a Comment

0 CommentsMAGAZETIBBC NEWS