Header Ads Widget

GAVU ATOA AGIZO KWA WAKUU WA MIKOA SERA YA AFYA KWA WAZEE

KATIBU wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa idara ya Organaizesheni Issa Gavu

Sehemu ya wajumbe wa baraza la wazee la CCM mkoa Kigoma wakiwa kwenye kikao cha baraza hilo lililofanyika mjini Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

KATIBU wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa idara ya Organaizesheni Issa Gavu amewataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kusimamia sera ya wizara ya afya ya uwepo wa chumba maalum kwa wazee na wazee kupewa kipaumbele wanapohudhuria matibabu kwenye vituo vya utoaji huduma za afya nchini

 

Gavu alisema hayo mjini Kigoma alipokuwa akizungumza na wajumbe wa baraza la wazee mkoa Kigoma akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo na kubainisha kuwa serikali imeshatoa mwongozo namna halmashauri zinavyopaswa kusimamia upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee.

 

Kutokana na hilo alisema kuwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wawasimamie wakurugenzi wa halmashauri ambao maeneo yao hayatekelezi maelekezo hayo wasimamiwe kwa karibu ili watekeleze maelekezo hayo ya sera ya afya nchini.

 

Pamoja na hilo alisema kuwa kwa sasa serikali inatekeleza mchakato wa mpango wa afya kwa wote ambapo tayari sera imeshapitishwa kwenye mamlaka zinazohusika na kwa sasa mchakato upo kwenye utungaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wote wakiwemo wazee.

 

Akizungumzia maagizo hayo Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye alisema kuwa wilaya zote za mkoa huo zina hospitali ya wilaya zikiwa na maeneo ya huduma za dharula na hospitali zote zina vyumba vya kuhudumia wazee.

 

Andengenye alisema kuwa ameongea na Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma, Dk.Jesca Leba  ambaye amemuhakikishia uwepo wa madirisha hayo na yanafanya kazi kwa mujibu wa taratibu za sera za wizara ya afya wakitekeleza maelekezo ya Raisi Samia kuhusu huduma za afya kwa wazee.

 

Awali mmoja wa wazee waliohudhuria kikao hicho,Juma Maulid kutoka wilaya Kibondo alisema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa kwa wazee kushughulikiwa kwa haraka wanapofika vituo vya utoaji huduma mambo ambayo yanaenda kinyume na mwongozo wa serikali katika upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI