Header Ads Widget

ZITTO AKEMEA MANYANYASO YA WANANCHI VIZUIZI VYA BARABARANI



Na Fadhili Abdallah,Matukio Daima App kigoma

KIONGOZI  wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amkemea tabi ya polisi na maafisa uhamiaji mkoani Kigoma kutumia  vizuizi vinavyowekwa barabarani katika maeneo mbalimbali ya barabara za mkoa Kigoma kutesa na kunyanyasa wananchi badala ya vizuizi hivyo kutumika zitumike kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Kabwe alisema hayo  akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya jumba la Maendeleo wilayani Kibondo akiwa kwenye mfululizo wa ziara ya mikutano yake mkoani Kigoma katika kuimarisha chama hicho kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Alisema kuwa serikali imekuwa na nia njema ya kuweka vizuizi hivyo kwa ajili ya kusimamia masuala ya usalama hasa kutokana na wakimbizi kushiriki kwenye vitendo vya uhalifu lakini watendaji wa polisi na vyombo vya ulinzi na usalama wametumia vibaya nafasi hiyo na kujinufaisha binafsi kwa kuwakamata wananchi wasio na hatia na kuwataka kutoa pesa na wasio na pesa wamepata mateso na manyanyaso makubwa.


kiongozi huyo wa chama alisema kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa vitambulisho vya utaifa kwa wananchi wa mkoa Kigoma ambapo  polisi na uhamiaji wanachukua changamoto hiyo kuwakamata na kuwadai pesa wananchi wasio na vitambulisho hivyo kwa kigezo kwamba watu hao siyo Watanzania hali ambayo ni manyanyaso makubwa kwa wananchi wa mkoa huo na kutaka jambo hilo likomeshwe.

Katika hatua nyingine Zitto ameitaka idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi kurudisha masoko ya pamoja baina ya wananchi wa mkoa Kigoma na wakimbizi wa Burundi katika Kambi ya Nduta wilayani Kibondo na kusema kuwa masoko hayo ni muhimu katika kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo.

Awali Waziri Kivuli wa viwanda na biashara wa ACT,Julius Masabo alisema kuwa sehemu kubwa ya wananchi wa wilaya ya Kibondo ni wakulima na biashara hivyo kuondolewa kwa masoko ya pamoja baina ya wakimbizi na wananchi wa wilaya hiyo kumeathiri uchumi wa wananchi hao kwa kiasi kikubwa.


Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya chama cha ACT Muhonga Ruhwanya akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe Mjini Kibondo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI