Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP Tanga
KAMATI ya kudumu ya Nishati na Madini ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha uvumi unaoenezwa wa uwepo wa uharibifu wa mazingira unaotokana na utekelezaji wa mradi wa Kimataifa wa Bomba la mafuta toka Hoima Nchini Uganda hadi Chongoleani-Tanga Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Dr David Mathayo walipotembelea mradi huo na kusema kuwa yapo madai yanayozungumzwa huko Duniani na hata watu toka nchi za Afrika Mashariki kuwa mradi huo ni mbaya kimazingira jambo ambalo sio la kweli.
Kamati ya hiyo ipo Mkoani Tanga kwenye ziara ya siku mbili ambapo imetembelea katika eneo la Chongoleani kukagua mradi wa bomba la mafuta toka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Tanzania ambapo mafuta ghafi yatasafirishwa kwenda nje ya Nchi.
"Tunaimani watu wanaopotosha kuhusiana na madhara ya kimazingira yatokanayo na mradi huu ni watu wasioitakia mema Tanzania,kutaka Watanzania wasifaidike na labda wamepewa pesa ili wauchafue mradi huu"Alisema Dr Mathayo.
Dr Mathayo aliongeza kuwa wametoa maelekezo kwa watekelezaji wa mradi huo EACOP kuwa wajikite katika maswala ya kijamii kama elimu,afya,maji n.k na kuongeza kuwa idadi ya watumishi toka katika eneo la mradi ambao idadi yao bado ipo chini na wapatiwe mafunzo kwa ajili ya maslahi ya utekelezaji wa miradi huo.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kamati hiyo limesema kuwa mradi huo ni muhimu kwa Watanzania, uwendelee na kamati hiyo inathibitisha kuwa hakuna madhara katika mradi huo hasa yale ya kimazingira.
Tunampongeza Rais Samia kwa kuendelea kuhakikisha kwamba mradi huo unakwenda vizuri na ifikapo Dec mwaka 2025 uwe umekamikika na kazi ya kuanza kusafirisha mafuta ghafi ianze.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Athumani Mbutuka alisema wamefurahishwa na kazi zinazoendelea katika mradi huo na kusema kazi kubwa ya Wabunge ni kuisimamia Serikali na imetoa maelekezo ya mambo ya msingi ya kuyafanya.
Aidha alisema kwa niamba ya Naibu Waziri Mkuu na Serikali wameyapokea maelekezo ya kamati hiyo na watahakikisha miradi yote ya maendeleo ambayo inafadhiliwa kwa dhana ya wajibu wa jamii kushiriki inaelekezwa katika maeneo yenye tija.
"Ni muhimu kutambua Serikali ya Dr Samia inavyiendelea kutekeleza majukumu yake katika mradi mbalimbali hapa Nchini "Alisema Mbutuka.
Alisema Dolla Mil 207 zimelipwa kati dolla 308 kwa ajili ya hisa za Serikali ya Tanzania, ajira 4228 zimetolewa kwa Watazania ambapo sawa na asilimia 91,Makampuni na watoa huduma 146 wametoa huduma katika mradi huo na kufanikiwa kujiingizia Shs Bil 355.
Mbutuka alisema bil 35 zililipwa kupitia fidia kwa wananchi waliopitiwa na mradi huo na kuongeza kuwa Tanzania ilikuwa na jukumu la kufanya kama Serikali na tumeendeleza kutekeleza majukumu na wataenda kutekeleza yote waliyoagizwa na kamati hiyo.
Hata hivyo Meneja wa eneo la mradi Mathiew Fayel alisema mradi huo unaendela vizuri na watumishi wapo katika eneo hilo la mradi kutekeleza majukumu yao kama kuandaa nguzo kwa ajili ya jeti itakapofunga meli na mategemeo mwaka 2025 mradi utakuwa umekamilika.
0 Comments