NA WILLIUM PAUL , SIHA.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Haji Mnasi (PhD) alisema kuwa, fedha hizo zilizotolewa Novemba mwaka huu ni kwa ajili ya miradi ya sekta ya Afya, Elimu msingi, Elimu sekondari.
Sekta nyingine ni pamoja na kununua vifaa tiba vya kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa jamii ambapo fedha hizo zimeelekezwa kujenga miundombinu mipya.
Alisema kuwa, mchanganuo wa fedha hizo ni ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa katika shule kongwe za msingi ambapo ni milioni 180, ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika shule ya msingi Sanya juu jumla ya shilingi milioni 28.
Aliendelea kudai kuwa miradi mingine ni ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi Ormelili milioni 128, ununuzi wa vifaa tiba hospitali ya wilaya, vituo vya Afya na zahanati milioni 900, ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati ya Mawasiliano na Mowonjamu milioni 100.
Miradi mingine ni ujenzi wa vyumba vya madarasa 48 katika shule 10 za sekondari kidato cha tano milioni 196, ujenzi wa matundu 125 ya vyoo katika shule 13 za sekondari kidato cha tano milioni 138, fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya mfuko wa jimbo milioni 58.2 pamoja na mfuko wa pamoja wa Afya (Health Social Basket Fund-HSBF) ili kuwezesha utekelezaji wa huduma za Afya katika vituo vya kutolea huduma milioni 64.3.
"Tunamshukuru na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hasani kwa jinsi ambavyo amekuwa akitujali wananchi wa halmashauri yetu ambapo ametupatia fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo na sisi tunamuahidi kuhakikisha tunasimamia fedha hizo kwa umakini mkubwa na thamani ya fedha iweze kuonekana kwenye miradi" Alisema Mkurugenzi Mnasi.
0 Comments