Na Diana Rubanguka, Kigoma.
Wanawake mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu, kujituma na kuwa na nidhamu katika utendaji ili kufikia malengo wanayojiwekea
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Ndaboine Dispensary iliyopo Mkoani Kigoma Daktari Abigael Kasumani wakati wa gafla ya kufunga mwaka kwa kikundi cha wanawake cha kisaidiana cha Faith kilichopo mkoani hapo.
Daktari Abigael alisema, pamoja na kuwa wengi wengi wao wameajiliwa na wengine kujiajili wasiridhike na mishahara, wafanye kazi binafsi za kujiongezea kipato lengo ni kukuza uchumi wa familia na Taifa kwa ujumla.
"Hakuna mtu aliyetajilika kupitia mshahara wa mwajili tufanye kazi binafsi, muda tunaotoka kwenye kazi za wajili tuutumie kufanya biashara ili kuongeza uzalishaji na kuinua vipato vyetu " alisema Dkt. Abigael.
Kwa upande wa mwanachama Anna Edward kutoka benk ya NMB tawi la Kigoma alisema, wanawake wanapaswa kuweka akiba za fedha wanazozizalisha lengo ikiwa ni kutatua changamoto za familia zinazoweza kujitokeza pamoja kukuza mitaji ya biashara kupitia fedha hizo za akiba.
Alisema kwa sasa kuna namna nyingi za kutunza fedha ambapo unaweza kufungua akaunti katika Benki yotote kwa kuwa kuna Benki mbali mbali hivyo kila Benki ina akaunti za kutunza kwa ajili ya kutoa kwa mwaka na zaidi.
"Kinamama tutunze fedha kwa ajili ya kukuza mitaji lakini pia kutatua changamoto zinazojitokeza katika familia zetu, tusiwe na matumizia mabaya yaliyo nje ya malengo yetu" alisema Edward
Kwa niaba ya wageni walikuwa kutoka vikundi mbali mbali vya kinamama vya kusaidiana mwekahazina wa kikundi cha Stong women Diana Rwegasira alitoa wito kwa wanawake kuepuka matumizi yasiyo ya lazima kwa kuwa ni chanzo cha kutotimiza malengo tarajiwa.
"Tumekuwa na tabia ya kununia vitu visivyo na ulazima, lakini pia tunatabia ya kuiga maisha ya jamii zinazotuzunguka ili hali vipato vyetu ni vya chini" alieleza Rwegasira
Kila mwanamke anapaswa kuwa na wivu wa maendeleo ili kila mmoja ajitume kwa kuiga mfano wa wanawake waliofanikiwa kuwa na kipato cha juu ambapo alisema siri ya mafanikio ni uvumilivu na kutokata tamaa.
0 Comments