Watu Wanne (4) Wamefariki Dunia, Wawili Wakiwa ni Familia Moja na Wengine Saba (7) Majeruhi Rufiji Mkoani Pwani Kijiji Cha Mloka Baada Ya Mtumbwi Waliokuwa Wakisafiria Wakitokea Shambani Kupinduliwa Na Kiboko Katika Mto RufijiKijiji Cha Mloka Kitongoji Cha Mpanga Mkoani Pwani. Waliofariki Dunia Ni WARDA ABDALLAH KITIMAI (Miaka13) Kidato Cha Kwanza Shule Ya Sekondari Mwaseni, Rakshmir Mwalami Makuka (Miaka 9) Mwanafunzi Wa Darasa La 2 Shule Ya Msingi Mloka, Sofia Musa Kilungi (Miaka 12) Mwanafunzi Wa Darasa La 4 Shule Ya Msingi Mloka,Hasani Musa Kilungi (10) Mwanafunzi Wa Darasa La 1 Shule Ya Msingi Mloka. Aidha We aliojeruhiwa Katika Ajali Hiyo ni Tatu Hasani Kiungulio (50), Samila Seleman Mdima(12) Mwanafunzi Shule Ya Msingi Mloka,Sefu Langi Mwanafunzi Wa Shule Ya Msingi Mloka Darasa La Tatu(3), Imani Uwesu Matendula (12) Mwanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza Shule Ya Sekondari Mwaseni,Shakmi Hamad Mwanafunzi Wa Darasa La Kwanza Shule Ya Msingi Mloka,Mudriki Athumani Mketo (6) Mwanafunzi Wa Shule Ya Msingi Mloka,na Fadina Salehe (ke 27) Mkazi wa Mloka. Mkuu Wa Wilaya Ya Rufiji Meja Edward Gowelle Akizungumxia tukio hilo licha Ya kutoa Pole kwa familia zilizokumbwa na mkasa huo ameomba Wananchi Kutotumia Mitumbwi Ya Asili Badala Yake Watumie Boti Za Kisasa Zilizowekwa kwaajili Ya Kusafirishia Watu. Aidha Pia aliwata kuacha Mara Moja Tabia Ya Kubeba Watu Wengi Katika Mitumbwi Hiyo. Aliwataka madereva wa mitumbwi hyo kuchukua tahadhari wakati wa kipindi hiki cha mvua za elnino zinazoendelea kunyesha katika maeneo tofauti hapa nchini.
0 Comments