Header Ads Widget

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA AGIZO TAKUKURU ...

  


NA HAMIDA RAMADHAN, MATUKIO DAIMA AAP DODOMA


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, George ameitaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuendelea kushughulikia watu wote ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya rushwa nchini bila kuangalia hali zao au vyeo vyao.


Simbachawene, alisema hayo leo jijini hapa, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU).


“Lazima tuwashughulikie watu wote wanaojihusisha na rushwa nchini zipo rushwa zinaoekana kabla ya kukamilika kwa miradi lakini zipo ambazo zinaanza kuonekana baada ya miaka mitatu tangu kukamilika kwa mradi hivyo wahusika wote wanatakiwa kukamatwa na kuhojiwa hata kama watakuwa wamestaafu”amesema


Na kuongeza "Hali hiyo itasaidia kukomesha tabia amabzo zimeluwa zikifanywa na watumishi wa umma kujihusisha narushwa na kuhama kituo cha kazi, " Amesema Waziri Simbachawene.


 Aidha Waziri Simbachawene, amekiri kuwa bado yapo malalamiko mengi ya wananchi kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika ofisi za umma hali inayosababisha wengi wao kushindwa kuzifikia huduma wanazozihitaji.


“Bado suala la rushwa ndogondogo ni tatizo sana kwa wananchi wetu na huko ndiko yapo malalamiko mengi ya watu kutokana na rushwa hiyo kuwanyima fursa ya kupata huduma, ".



Na kuongeza“Huduma hizo ni pamoja na elimu ngazi za chini kati hadi vyuo vikuu, lakini pia huduma za afya,kodi na leseni ambako kumewekwa utaratibu mgumu na ukilitimba katika utoaji wa huduma ili tuu watu watoe rushwa ndipo wahudumiwe”amesema Simbachawene


Aidha, ameeleza kutokana na hali hiyo kila taasisi inatakiwa kutengeneza mkataba wa huduma kwa wateja na TAKUKURU iwe nao kama sehemu ya kufuatilia utekelezaji wake.


“Tukitoka tuu hapa tukaenda pale hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma General tukajificha mahali na kuangalia namna shughuli zinavyoendelea kama ni muhudu au daktari atakuwa anatoa huduma bora tutaona na kama kuna muhudumu ambaye atakuwa hatoi huduma bora tutabaini hivyo hizi rushwa ndogondogo zinakera sana wananchi kuliko hata hizi za ubadhirifu wa mabilioni ambayo wao hawayaoni”amesisitiza Simbachawene



Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Rashid Hamduni amesema, mkutano huo ni wa siku tatu ambapo lengo lake ni kujadili mafaniko na changamoto kwa mwaka uliopita ili kuzipatia suluhu.


Hamduni, amesema katika kipindi cha mwaka uliopita taasisi hiyo, imeokoa kiasi cha Sh. bilioni 171.9 ambazo zingeingia mifukoni mwa watu kama TAKUKURU, isingefanya oparesheni mbalimbali kwenye miradi ya umma.


Hata hivyo, amesema mkutano huo utatoka na maadhimio ambayo watakwenda kuyafanyia kazi ili kupunguza malalamiko ya wanachi kuhusu vitendo vya rushwa katika sehemu mbalimbali nchini.



Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI