Header Ads Widget

WANAUME 144 IRINGA WAKIMBILIA POLISI KISA KUFANYIWA UKATILI KATIKA NDOA

 

Na Matukio Daima App 

IDADI ya wanaume 144 mkoani Iringa wamefika Polisi kati ya mwaka 2020  hadi 2023  kulalamika kufanyiwa vitendo vya Ukatili kwenye Ndoa.

Mbali ya idadi hiyo ila inaelezea kuwepo kwa idadi Kubwa zaidi ya wanaume ambao wanapigwa ama kufanyiwa Ukatili na wanawake kwenye Ndoa ila wamekuwa wakiona aibu kwenda Polisi kuripoti Ukatili huo.



Kamanda   wa  polisi  wa  mkoa wa  Iringa  Allan Bukumbi aliyasema  hayo   wakati  akifungua kampeni   iliyoandaliwa  na  dawati la  jinsia  wanawake na  watoto  kwa  ajili ya kuadhimisha    siku  16  za  kupinga  ukatili  wa  kijinsia  alisema  kuwa 
takwimu zinaonesha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha matukio kwa wanawake na watoto na yanaonesha umuhimu wa kuendelea na kampeni hii. 

Kuwa takwimu zinaonesha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha matukio kwa wanawake na watoto na yanaonesha umuhimu wa kuendelea na kampeni hii. 

Alisema dadi ya Watoto waliofanyiwa ukatili  mwaka 2020 ni 629, mwaka 2021 ni 539, mwaka 2022 ni 529 na mwaka 2023 Januari hadi Oktoba 490  Wanawake kwa mwaka 2020 ni 501, mwaka 2021 ni 611, mwaka 2022 ni 516 na mwaka 2023 Januari hadi Oktoba ni 349 Aidha kwa upande wa Wanaume mwaka 2020 ni 36 mwaka 2021 ni 31, mwaka 2022 ni 26 mwaka 2023 Januari hadi Oktoba ni 49 kuwa idadi inaongezeka yaweza kufika 144 ama zaidi  kwani elimu ya Ukatili inaendelea kutolewa


Japo  bado tatizo lipo kwenye jamii hasa kwa kundi la wanawake na watoto japo kua wanaume wamekua hawana desturi za kuripoti matukio yanayowahusu ila  jeshi la  polisi limepanga  kutowaacha kwenye elimu  itakayoendelea  ili  kuwahamasisha kujitokeza kuripoti matukio ya ukatili.


"Utoaji wa elimu utajikita katika kupambana na vyanzo vinavyosababisha vitendo vya ukatili kama vile; uelewa mdogo, Mila na desturi potofu, ulevi, imani za kishirikina, makuzi na malezi, utandawazi, migogoro ya kifamilia " alisema  Bukumbi 

Kuwa  Chimbuko  la maadhimisho ya siku kumi na sita (16) za kupinga ukatili wa kijinsia ni la kimataifa, yaliyotokana na mauaji ya kikatili ya wasichana wa Mirabelle huko nchini Dominica. 

Kuwa mauaji hayo yalifanyika mwaka 1960 Kutokana na hali hiyo mwaka 1991 umoja wa mataifa ulitenga siku 16 kuanzia Novemba 25 (International Day of No Violence Against Women) kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wananwake huku kilele cha kampeni hii huwa ni Disemba 10 ambayo ni siku maalumu ya kuadhimisha tamko la haki za binadamu.

" (International Human Rights Day) Mnamo mwaka 1996 Tanzania ilianza rasmi maadhimisho haya ikiwa ni sehemu ya kuungana na nchi zingine duniani kupinga ukatili wa kijinsia ambao umekua changamoto kubwa katika jamii" 

Kuwa  lengo la kampeni hii kuongeza ushawishi, kubadilishana taarifa na uzoefu, kujenga uwezo wa pamoja, matumizi mazuri ya rasilimali zinazopatikana na kuunganisha nguvu za asasi za kijamii katika kuhamasisha, kuelimisha, kukemea na kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa kijinsia kwa jamii.


Hivyo  Jeshi la polisi Mkoa wa Iringa kupitia kamisheni ya polisi jamii limeandaa shughuli za utoaji elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni hii kwa kushirikiana na wadau.

 Kamanda  Bukumbi  alisema  kuwa  mwaka  huu  wamekuja na Elimu iliyobeba kauli mbiu ya mwaka 2023 Wekeza kuzuia ukatili  wa  kijinsia .

Alisema  Katika Mkoa wa Iringa kumekuwepo na matukio ya ukatili wa kijinsia na watoto kama vile Mauaji, ubakaji, ulawiti, Mimba kwa wanafunzi, kuzini na maharimu, kutelekeza watoto, ndoa za utotoni, kuangamiza watoto wachanga,shambulio la kudhuru mwili, kujeruhi na  ukatili  mwingine tofauti .


Kwa  upande  wake  Mkaguzi  wa  polisi  mkuu  wa  dawa la jinsia  wanawake na  watoto  mkoa  wa  Iringa  Elizabet Swai  alisema  kuwa   wamejipanga  kutoa  elimu  kwenye makundi mbali mbali likiwemo  kundi la  vijana  wa  pikipiki  za  miguu miwili (boda  boda ) ,bajaji ,daladala   pia  kupita kwenye  kumbi za  starehe  kuwakamata   wazazi  wanaokwenda na  watoto lakini pia kutoa  elimu ya ukatili wa kijinsia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI