Steven Meo Mwasumilwe ambaye ni Wakala wa kukusanya ushuru Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kughushi .
Mtuhumiwa huyo amefikishwa Octoba 30 mwaka huu katika Mahakama ya Wilaya Rungwe, mbele ya Hakimu Mwinjuma Bakari Banga .
Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 04/2023, Jamhuri dhidi mtuhumiwa huyo ameshtakiwa kwa kosa la kugushi stakabadhi zenye kiasi cha Sh. 330,000/= mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Ilidaiwa kuwa Bwana Mwasumilwe alikusanya fedha za Ushuru wa Mazao na kufuja fedha hizo Kwa kutoa stakabadhi za kugushi baada ya hapo alizitumia fedha hizo kwa matumizi yake binafsi.
Kosa hili ni kinyume na kifungu cha 335(a) cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16(RE: 2022)
Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake amerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana na shauri limepangwa kutajwa tena Novemba 13, 2023 kwa kuwa uchunguzi bado haujakamilika
0 Comments