Header Ads Widget

UTUMIKISHWAJI WA WATOTO WAONYWA NJOMBE DC

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe
Baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe
xxxxzz

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wazazi na walezi wilayani Njombe wametakiwa kuacha tabia ya kuwapeleka kufanyakazi za ndani na kuwatumikisha watoto waliohitimu elimu ya msingi na wanaotarajia kuhitimu kidato cha nne kwani kasi ya kuporomoka kwa maadili ya kiafrika imekuwa kubwa.


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli ametoa rai hiyo katika kikao cha baraza la madiwani ambapo amesema ongezeko la watoto hao uraiani lisitumike kuwatumikisha katika kazi za ndani  na badala yake wasubiri mpaka watakapoendelea na masomo hapo Januari 2024.


Baadhi ya madiwani akiwemo Neema Mbanga,Getruda Chungwa na Javan Ngumbuke wamesema kutokana na changamoto kubwa ya kuporomoka kwa maadili barani afrika ipo haja ya kuwalinda watoto wasije tumbukia kwenye wimbi la ukatili.


Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya wazazi wilayani Njombe akiwemo Ester Mhoka na Clemence Luwanja ambao wamekiri kuwapo kwa baadhi ya wazazi ambao bado wanawapeleka watoto kufanya kazi za ndani katika mikoa mbalimbali jambo ambalo linapaswa kupingwa kwa nguvu zote.


Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoa iliyotajwa na Rais wiki iliyopita kuwa una ongezeko kubwa la watoto wanaopata ujauzito hatua ambayo kila mzazi anapaswa kumlinda mtoto.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI