Header Ads Widget

MATUMIZI HOLELA YA DAWA ZA ANTIBIOTIKI KUCHANGIA USUGU WA DAWA

Na Hamida Ramadhani  Matukio Daima App Dodoma

MKURUGENZI wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga, amesema matumizi holela ya dawa za antibiotiki yanachangia kwa kiasi kikubwa tatizo la usugu wa dawa kwa wanyama na binadamu.


Prof. Nonga amebainisha hayo kwenye mkutano wa siku moja uliowakutanisha wataalam kutoka wizara ya Mifugo na taasisi zake, Ofisi ya Waziri mkuu,wizara ya Afya na wawakili wa wanyama pori.


Kikao hicho kilikuwa na lengo la kujadili mradi ambao utajikita katika kuangalia uelewa wa wananchi hasa wafugaji kuku kuhusu usugu wa vimelea kwenye dawa za antibiotiki ambavyo hivi sasa umetoka kwa wanyama na kuhamia kwa wanadamu.


Amesema mradi huo ambao utakwenda kutekelezwa katika mikoa ya Kilimanjaro na Mwanza unalenga kwenda kufanya tafiti kwa wafugaji wa kuku kama wanatambua chanzo cha usugu wa dawa katika mifugo yao.


“Matumizi ya dawa yasiyo sahihi kwa kuku hawa wa kisasa imekuwa ndiyo chanzo cha usugu wa vimelea vya magonjwa hasa matumizi ya dawa za antibiotiki kwa uzalishaji wa kuku.


“Mradi huu utakwenda kutekelezwa katika mikoa hii ya Mwanza na Kilimanjaro nitoe wito wangu kwa wafugaji kuku na watumiaji wengine wa mazao ya kuku kutoa ushirikiano ili matokeo yatakayotoka yatoe majibu yatakayo saidia wafugaji na serikali kupambana na changamoto ya usugu wa vimelea kwenye dawa”amesema


Kadhalika, amesema matokeo ya utafiti huo yatasaidia jamii kuwa salama dhidi ya usugu wa vimelea hasa pale wafugaji watakapo punguza matumizi holela ya dawa za antibiotiki kwa kuku.


Aidha, alisema sababu za kupeleka mradi huo katika mikoa hiyo ni kuwa na idadi kuwa ya wafugaji kuku wa kisasa ambao wanamatumizi makubwa ya dawa zinazosababisha usugu wa dawa.

Naye, Mhadhiri wa chuo kikuu cha cha Sayansi St. Francis Ifakara Filbert Madoshi, alisema matumizi ya dawa yasiyo zingatia maelekezo ya wataalam yamekuwa chanzo cha vimelea kujenga usugu wa dawa.


Amesema hivi sasa jamii imekuwa na tabia ya matumizi ya dawa ambayo hayazingatii maelekezo ya wataalam wa afya hali ambayo kama haitafanyiwa kazi hakutakuwa na dawa ambazo zitatumika kutibu magonjwa yaliyopo.


“Kikukwa kinachotakiwa ni jamii kubadili tabia ya matumizi holela ya dawa hasa antibiotiki dawa zilizopo zitashidwa kutibu magonjwa yaliyopo kutokana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa.


“Unakuta mtu ametoka safari kichwa kinauma kwa uchovu ananunua dawa anameza bila kupata ushauri wa wataalam lakini pia mtu anaweza kupewa dozi ya siku tano yeye anatumia siku tatu bila kujali kuwa kuna baadhi ya vimelea vinaweza kuishi na kujenga usugu wa dawa”alisema


Hata hivyo, kupitia mradi huo alisema watakwenda kuangalia uelewa wa jamii kama inao ufahamu wa tatizo la usugu wa vimelea kwa wanayama na binadamu.

Pia Mratibu wa Taifa wa maswala ya Usugu wa vimelea dhidi ya dawa Emiliana Francis kutoka wizara ya Afya alisema lengo la mkutano ni kujadiliana kuhusu namna ya kuratibu usugu wa vimelea dhidi ya dawa ikiwa chini ya wizara ya afya kupitia mradi wa Inika ambao umewakutanisha ili kuweza kujadiliana hususani maeneo wanayotaka kuyafanyia kazi


“Tunajua kwamba katika jamii kwa mfano mfugaji wa kuku au wafugaji wa ng’ombe wanatumia sana hizi dawa za Antibiotiki katika kutibu wanyama wao kwaio na tunajua kwamba wanapotakiwa watumie hizi dawa katika kutibu wanyama wanatakiwa watoe muda fulani ambao hizi dawa zinakuwa zimeisha ndani ya mnyama kwaio ndio tunatakiwa sasa kama ni kuku ndio tumle pale”


“Mradi wao umejikita katika maeneo ya kupunguza au kuzuia usugu wa vimelewa dhidi ya dawa kwenye upande wa kuijengea jamii uelewa kupitia kile chakula tutakachokula kwaio hawa wenzetu wametukutanisha leo hapa katika hii JUKWAA (Platform)  wanataka kwenda kuielimisha jamii  kuhusiana na maswala ya usugu hasa kwenye maswala ya kuku kwenye maswala pia ya wafugaji kuhusiana matumizi holela ya dawa za Antibiotiki”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI