Header Ads Widget

MCHUNGAJI MSIGWA AMSHUKIA MAKONDA "HANA MAMLAKA YA KUMUAGIZA WAZIRI MKUU"

IKIWA  ni  siku  mbili  toka  katibu  wa itikadi na uenezi  wa  chama  cha  mapinduzi (CCM) Taifa  Paul Makonda  kutoa  agizo la miezi  sita  kwa  waziri  mkuu wa jamhuri ya  muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  kutatua  kero  ya  ardhi  nchini , mwenyekiti  wa  chama  cha Demokrasia  na maendeleo (CHADEMA)  kanda ya Nyasa  mchungaji  Peter  Msigwa amesema agizo  hilo  ni  kinyume na katiba ya  nchi kwani  waziri mkuu anagizwa na Rais  sio  wasemaji  wa  vyama.

Akizungumza na  Matukio Daima Media leo  mjini Iringa kuhusu maoni yake  juu ya agizo  la  Makonda  kwa  waziri mkuu na mawaziri nchini ,mchungaji Msigwa  alisema  kuwa  amesikitishwa na jinsi ambavyo katiba ya  nchi  inavyovurugwa na msemaji  wa CCM kwani  kazi ya msemaji  si  kumuagiza  waziri mkuu ama  waziri  yeyote  ndani ya nchi  kwani  mawaziri  wapo  kikatiba na katiba  na  nchi inaongozwa na katiba  ya  nchi  sio  katiba za  vyama .

“ Nasikititika  sana   kuona  watanzania  waliwengi hawapendi  kusoma  katiba   yetu  na  ndio maana  kwa sasa baadhi ya  watu  wanashangilia  matamko  ya  Makonda  kwa  waziri  mkuu na  mawaziri  anafanya  haya  kinyume kabisa na katiba ya  nchi  yetu  kewani  waziri  mkuu na baraza la mawaziri  limetajwa  kwenye katiba ya  jamhuri ya muungano  wa Tanzania   waziri mkuu ni kiongozi wa  heshima   kama  kuna matatizo yao ndani ya  CCM waongee  ndani ya  vikao  vyao  sio  nje ya  chama “ alisema  Mchungaji Msigwa .

 

Alisema  kuwa  kwenye katiba  ya nchi  hakuna  sehemu  ambayo  imetaja  Mwenezi wa chama  chochote  cha  siasa    hivyo  ni  wazi  waziri  mkuu ama mtumishi  yeyote wa  serikali anapaswa kuheshimiwa  bila  kujali anatokana na  chama  gani  cha  siasa .

 

Hata   hivyo  mchungaji  Msigwa  alisema  mbali ya katiba  ya  jamhuri ya  muungano  wa Tanzania   kutowatambua  wenezi  wa  vyama  vya  siasa  ila  hata katiba  yao  CCM hakuna  sehemu  ambayo inampa nguvu  Mwenezi wa  chama  kumuagiza  waziri  mkuu ama  waziri  yeyote  zaidi ya  kukisemea  chama  chake .

 

Alisema ndani ya  katiba  yao  CCM  kazi ya  idara ya  itikadi na  uenezi  imeeleza  wazi  majukumu yake  ambayo ni    kueneza  na  kufafanua itikadi  na sera  za  CCM , kupanga  na kusimamia mafunzo na  maandalizi ya  makada na  wanachama ,kusimamia  vyombo vya habari  vya  chama ,mawasiliano na uhamasishaji wa umma kwa  ujumla  ,kuongoza na kusimamia  maandalizi ya  Programu na ilani  za uchaguzi  za  CCM  , Kusimamia utafiti ,maktaba na  nyaraka  za  CCM pamoja na  kushughulikia masuala ya  msingi  ya  itikadi na  sera  za  CCM  na  si vinginevyo .

“ Hii ndio kazi ya  Mwenezi  sio  kutoa matamko hana mamlaka  hiyo  nadhani  alikuwa anapiga  porojo  na  kwa  kuwa  watu  wengine  hata  wana  CCM wengi  hawajui  anamuita  mkuu  wa  mkoa  pale kama  mtoto  ana muita  waziri kama  mtoto  hii  ni kinyume na  tusitengeneze  utamaduni kama  huu  mtu  ambae  hana mamlaka  kutoa  kauli kama  hizi “alisema Mchungaji  Msigwa

Kuwa  hana  ugomvi   wowote  na  Makonda  ila   hakubaliani  ni  njinsi  ambavyo Makonda  anavyotaka  kuvuruga  katiba  ya  nchi  na  kujipa madaraka  makubwa  ambayo  katiba  haimtambui kwani  mwenye  mamlaka  ya  kumuagiza  waziri mkuu ama  waziri  yeyote ni  Rais  wa Jamhuri  ya  muungano  wa Tanzania  na  sio  vinginevyo.

Pia  alisema  anashangazwa  na tabia  iliyozuka  ndani ya  CCM ya  viongozi  wa chama  kufanya  ziara ya  kukagua  miradi  wakati wanao  wawakilishi  wa wananchi kwa maana ya  Rais ,mbunge na diwani  ambao  ndio   wanapaswa  kusimamia  miradi na  kuwasilisha  taarifa  ya utekelezaji  wa miradi  hiyo  kwenye  vikao  vya  ndani  vya  chama  ambako huku  wanaweza  kuwahoji  hata  mawaziri ila  sio  kutoka  hadharani hivi .

Hata  hivyo  alisema  kinachoendelea  ndani ya  CCM kwa  sasa ni kama  wajenzi  wa mnala wa Babeli jambo  mbalo kwao  upinzani  wanaanza  kuona  wazi  ni namna gani  ambavyo  CCM inakwenda  kuachia madarakana  kwani japo  wao  wanafurahia  ugomvi  wao  wa ndani  kuja  hadharani kama  hivi kwa  kuonza  kuonya  wastaafu wao.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI