Header Ads Widget

TMEA YAWATAKA WANUFAIKA WA MRADI WA 'SAUTI YA MWANAMKE SOKONI' KUTOIPA KISOGO TEKNOLOJIA

  

Na: Mtukio Daima App 

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Bi.Monica Hangi amewahasa Wanawake ambao ni wanufaika wa programu ya Mwanamke Sokoni ambayo inaratibiwa taasisi isiyo ya kiserikali ya Equality for Growth (EFG) kutumia vyema teknolojia katika kutanua masoko.


Akizunguza katika maadhimisho ya miaka 15 tokea kuanzishwa kwa taasisi ya EFG, ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) leo Oktoba 31, 2023, amesema kuwa teknolojia inakuwa hivyo ni wakati wa kwendana na kasi hiyo ili kuepuka kuachwa nyuma.


Pia amewataka Wanawake ambao ni wanufaika wa programu hiyo kuepuka ku huku mikopo ambayo inawaletea matatizo na kuwadidimia maarufu kama 'mikopo ya kausha damu "Tuchukue mikopo inayotunufaisha kutoka hatua moja kwenda nyingine"


Ameongeza kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwenye taasisi ya EFG kwa lengo la kuwainua Wanawake sokoni ili waweze kuinuka kiuchumi.


Aidha Mwenyikti wa Bodi ya EFG, kwa niaba ya taasisi ameeleza baadhi mafanikio mbalimbali ambayo wameyapata katika kipindi cha miaka mitano.


"Program ya Mwanamke Sokoni imetengezwa katika mikoa tisa ya Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Mwanza, Shiyanga, Lindi, Mtwara, Mbeya, Iringa Tanga katika Wilaya ya Lushoto na Mkoa wa Mara..., lengo letu fursa hii tunataka ifike kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara"amemesema wa Bodi ya EFG

 Ameongeza kuwa "Kupitia programu hii imemuwezesha Mwanamke kushika nafasi za uongozi sokoni na kongeza ujuzi na kusaidia Wanawake kujiamini katika kuongoza kwenye nafasi mbalimbali"






Katika maadhimisho hayo ambayo yameudhuriwa na watu zaidi ya 200 hususani Wanawake ambao ni viongozi wa masoko mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Dar es salaam, Mwakilishi kutoka taasisi ya Digital Brain ametumia nafasi hiyo kuwasihi Wanawake juu ya umuhimu wa teknolojia katika kukuza biashara zao, ambapo amesema kuwa kutoendana na teknolojia kunaweza kuleta utofauti mkubwa baada ya miaka michache ijayo kwamba waliotumia vyema fursa ya teknolojia wanakuwa katika nafasi nzuri ya kuwaacha nyuma wale ambao wameshindwa kwendana nayo.


Taasisi ya EFG imekuwa ikishughulika na kuwainua Wanawake kiuchumi hususani walioko masokoni na kuchochea mabadiliko ya sheria ili kuwawezesha Wanawake kuendelea kuinuka kiuchumi na kukuza masuala ya kijinsia hususani Wanawake kuwa sehemu ya uongozi katika ngazi mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI