Header Ads Widget

ALIYEKUWA DC MONDULI, FESTO KISWAGA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI

 

NA MATUKIO DAIMA APP.

IRINGA.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga na kada wa Chama cha Maapinduzi CCM amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Isimani Mkoani Iringa.

Akizungumza na wanahabari Mkoani Iringa mara baada ya kuchukua fomu ya ubunge amesema kuwa amejipima na kuona anatosha kuomba ridhaa chama chake kiweze kumfikiria kumpa nafasi ya kuwa Mbunge wa jimbo la Isimani.

Alisema kuwa dhamira yake ya kugombea ubunge katika jimbo hilo ni kuwaletea maendeleo wakazi wa Isimani, hususani kupitia maboresho ya sekta ya kilimo.

"Nimeamua nakuona natosha na kuomba miongoni mwa vijana, wazee akina mama na watoto kutokana na recodi yangu ya uongozi, hivyo kutokana na mahitaji ya sasa ya wananchi wa Isimani nimejipima na kuona natosha kwa sababu mimi ni msikivu wa wananchi"

Festo Kiswaga awali aliwahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara,Mkuu wa Wilaya Mvomero,Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu,Mkuu wa Wilaya ya Kahama na baadae Wialaya ya Monduli.

kiswaga alisema kuwa Kutokana na uzoefu huo nafahamu mahitaji ya wananchi wa Isimani kwa sababu wananchi hao wamekosa mahitaji yao kutokana na kutosikilizwa kwa ukaribu.

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI