Header Ads Widget

HUKUMU YA MAJANE WA NYAMA YA SWALA ,TLS IRINGA YAWASILISHA BARUA YA RUFAA MAHAKAMA KUU KANDA YA IRINGA

 


NA MATUKIO DAIMA APP

CHAMA cha mawakili Tanganyika (TLS) mkoa wa Iringa kimewasilisha mahakama Kuu Kanda ya Iringa barua ya rufaa (  Notice of Appeal  )  kwa ajili  mjane  Maria Ngoda aliyefungwa jela miaka 22 kwa kosa la kukutwa akiuza vipande 12 vya nyama ya Swala kinyume na Sheria .

Huku mawakili 10  kati yao akiwemo Wakili mwanamke Jane Massey na Wakili Mchungaji Joshua Chusi wakiwa miongoni mwa jopo la mawakili watakaomtetea mjane huyo .

Mwenyekiti wa TLS mkoa wa Iringa Moses Andimbwile akizungumza na Matukio Daima Media Jana  kuwa  hadi sasa tayari imekwisha andikwa barua ya rufaa (  Notice of Appeal  ) ambayo tayari imeshafailiwa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Iringa  tangu Novemba 8 2023. 

Alisema kuwa Kinachofuatia sasa hivi ni kufaili mahakamani hati ya Rufaa (Petition of Appeal) ambapo hadi jana usiku jopo la Mawakili 10 kutoka TLS Iringa walikuwa wamejifungia kuandaa sababu  za rufaa hiyo.

Hati hiyo ya Rufaa inapelekwa mahakamani jumatatu yaani Novemba 13 mwaka huu  2023.

Alisema mwitikio wa mawakili wa kujitolea kumsaidia mjane huyo katika rufaa yake umekuwa mkubwa zaidi kwani hadi sasa mawakili 10  wamejitokeza .

"Mawakili wafuatao watahusika katika maandalizi yote ya rufaa hadi usikilizwaji  Moses Ambindwile,  Dr. Rwezaula Kaijage, Frank Ngafumika,  Barnabas Nyalusi, Jane Massey, Samson Rutebuka, Wakili Mchungaji  Joshua Chusi,Innocent Kibadu, Cosmas Kishamawe na Jali Mongo"

Andimbwile wanaendelea na  jitihada zao juu ya kumtetea Maria Ngoda kwa kuendelea na utafiti juu ya kesi hiyo Pamoja kuandaa sababu za rufaa ili kufikia jumatatu ziweze kuwasilishwa mahakamani ambazo baada ya hukumu kutolewa ni siku 45.

 Hivyo kutaka jamii na umma wa watanzania, ambayo imeguswa kihisia, wanapaswa kuwa na Subira, kwani mchakato wa Rufaa unaendelea na kusubiri kuona mahakama itatenda nini kwa kujua kama ilimuonea mhusika au haikumuonea.

Wakili alisema kuwa, wananchi waendelee kuwa na uvumilivu, kwani kilichofanywa na mahakamani kwa mujibu wa sheria, kwani sheria hiyo hiyo ndio imetoa nafasi ya rufaa, na kwa kuwa imeshaanza kutekelezwa basi wananchi wataona kitakacho jiri mbele ya mahakama.


Kwa upande wake Wakili Emmanuel Chengula alisema kwa mtazamo wake wa  jumla kuhusiana na suala hili, Pamoja na kwamba taratibu za ukataji rufaa zinaendelea, yapaswa kutegemea kile kitakacho amuliwa mahakamani ndio utakao kuwa ni uamuzi sahihi kwa kutegemea na majadiliano ya pande mbili za mawakili watetezi wa TLS na Upande wa Mahakama.

 Juu ya mfanano wa kesi kwa kulinganishwa na kesi ya malkia wa pembe za ndovu ya mwaka 2019, iliyotolewa hukumu katika mahakama ya kisutu Wakili  Chengula alisema zote ni kesi za uhujumu uchumi lakini ni kesi mbili tofauti, ambapo katika kesi ya kwanza ya malkia wa pembe za ndovu, kulikuwa na Plea barganining, ambayo yalihusisha majadiliano ya awali yaliyofanywa baina ya malkia wa pembe za ndovu na DPP, ambapo mahakani hukumu yake ndio ilikuwa ya kulipa faini na akapaswa kulipa faini ya mahakama Pamoja na makubaliano yaliyofanyika katika plea bargaining. 

 Wakati  kesi ya huyu mama wa nyama ya swala utofauti wake Zaidi ni kuwa hakukuwa na plea bargaining (hakukiri makosa ya kuandikishana na kulipa fidia), hivyo alikiri akiwa mahakamani na huku ikatolewa hukumu sawa na shauri lilivyosikilizwa.

"Plea Bargaining Inafanyika wakati  wowote hata kama kesi imeanza kusikilzwa, ambapo anayeshtakiwa anaweza kuonyesha nia ya kutaka kukiri mashtaka ili waweze kuandishikiana, na sawa na uzoefu plea bargaining haiwezi kufanyika baada ya  hukumu, kutokana na Ushahidi ulishafikishwa mahakamani hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa kosa lililothibitishwa"

Kuhusiana na uthibitisho wa Nyama aliyokutwa nayo mhusika hupimwa na wataalamu wanaohusika,  ambapo sampuli huchukuliwa na Kwenda kupimwa kama kuna utata kwa nyama inayouzwa sawa na mazingira. 

Alisema katika kukata rufaa haiwezekani kuomba uthibitisho wa usahihi wa nyama ya swala labda kama katika kusikilizwa kwa kesi kuna hoja ya aina hiyo iliibuka na haikutiliwa maanani, hapo inaweza kupelekea kuonesha kuwa mhusika alifungwa bila utaratibu, sawa kwani kuna hoja haikufafanuliwa bayana kuhakikisha kila kitu kinakwenda .


Hukumu dhidi ya Maria Ngoda ilitolewa Novemba 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha  kuwa ni kweli mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000 kinyume na Sheria .

Akitoa hukumu hiyo kwa mjane huyo mkazi wa Zizi la Ng’ombe mjini Iringa, Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, Mkasiwa alisema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 86 (1) (2) (c) cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba tano ya mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho na kifungu cha 59 (a) (b) cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2016.

Wakati akijitetea bila usaidizi wa wakili  mjane huyo alikiri ni kweli alikutwa na ndoo yenye nyama hiyo ambayo alidai alikabidhiwa na mtu aliyemtambua kwa jina moja la Fute bila kujua ina nyama ya nini .

Alisema alilazimishwa abebe ndoo hiyo na kufikishwa kituoni na kufunguliwa kesi ya kukutwa na nyara za serikali sambamba na kosa la uhujumu uchumi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI