Header Ads Widget

TASWO : TUHESHIMU TOFAUTI ZETU ZA MAUMBILE

 


NA ARODIA PETER,MATUKIODAIMA App

DAR

Wataalam wa masuala ya jamii wametoa rai kwa Watanzania kuheshimu tofauti za maumbile ili kuweza kupitia hatua za pamoja za kijamii.


Hii ni kauli mbiu ya wanataaluma hao watakayoitumia katika Mkutano mkuu wao unaotarajiwa kufanyika Jijini Mbeya Novemba 14 hadi 16 mwaka huu huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Novemba 11,2023, Makamu mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO), Salma Fundi, alisema wameamua kutumia kauli mbiu hiyo mwaka huu wakisisitiza umuhimu wa kuheshimu tofauti za watu kiitikadi, kidini, kikabila na jinsia katika jamii.


“Hii ina maana kwamba wataalam wa Ustawi wa jamii tunaamini kwamba ni muhimu kuheshimu tofauti za watu na tunaweza kufanya hivyo kwa kuchukua hatua za pamoja za kijamii.


“Lakini tunaamini kwamba tofauti zetu zinaweza kuwa chanzo cha nguvu za maelewano, kwani tunapoheshimu tofauti za kila mmoja tunaunda jamii yenye amani na umoja zaidi.


Fundi aliongeza kuwa mkutano huo utahusisha wizara zote zinazosimamia huduma za ustawi wa jamii, idara mama ya ustawi wa jamii, wataalam wa ustawi kutoka sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali, mashirika ya kiraia na vyuo vikuu.


Aidha wataalam hao watajadili mada mbalimbali za ustawi wa jamii ikiwa ni pamoja na watoto na vijana, wazee, watu wenye ulemavu, unyanyasaji wa kijinsia pamoja na umasikini.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI