Na,Jusline Marco:Arusha
Waziri wa maendeleo ya jamii,Jinsia, wanawake na makundi maalumu Mhe. Dkt.Dorothy Gwajima amezitaka Taasisi za elimu na vyuo kuzalisha Wataalamu wenye uwezo wa kujiajiri na wanaokubalika katika soko la ajira .
Dkt. Gwajima ameyasema hayo Jijini Arusha wakati akifungua Kongamano la siku tatu la Wataalamu wa maendeleo ya jamii na miaka 60 ya Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru ambapo amesema mustakabali wa maendeleo kwa Taifa lolote Duniani inategemea mchango wa vyuo na Taasisi za mafunzo katika kuandaa Wataalamu mahiri na wenye weledi ambao ndio chachu ya kuleta mageuza ya kifikra na Maendeleo jumuishi na endelevu kwa jamii.
Aidha amesema Mafunzo yanayotolewa ni sharti ya akisi na kwenda sambamba na mipango ya nchi na vipaumbele vya jamii na Wadau ili kueleta matokeo chanya ya maendeleo ambapo wizara pia imeandaa muongozo wa uanzishwaji na uendeshaji wa majukwaa ya uwezeshwaji wanawake kiuchumi na kupitia muongozo huo majukwaa 3091 yameanzishwa kutoka mwaka 2022 hadi kufikia April 2023.
Vilevile ameongeza kuwa majukwaa hayo husaidia kuwakusanya wanawake pamoja ili kupata elimu ya ujasiriamali na fursa za mitaji ya kuanzisha biashara pamoja na kupata taarifa kuhusu masoko ya bidhaa zinazozalishwa kwani majukwaa hayo ni shamba darasa ambapo kila mwananchi anatakiwa kuyajua na kunufaisha familia nzima.
Ameeleza kuwa wafanyabiashara ndogondogo ni kundi mojwapo linalochangia uchumi wa taifa na kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira ambapo amewataka wataalamu wa maendeleo ya jamii walio katika sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kupitia ofisi ya rais TAMISEMI kuratibu na kusimamia afua zote zitakazowezesha kundi la wafanyabiashara ndogondogo kukua kiuchumi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya uendeshaji ya Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru Dkt. John Lusingu amesema moja ya jukumu walilopewa ni kuhakikisha Taasisi inayosimamia jukumu la maendeleo ya jamii kuipeleka katika Karne iliyopo Sasa ya teknolojia na maendeleo ambayo yanabadilika kila siku .
Ameongeza kuwa lengo la Kongamano hilo ni kutambua mchango wa taaluma wa maendeleo ya jamii nchini katika kuchochea maendeleo endelevu na jumuishi huku kauli mbiu ikiwa ni sekta ya maendeleo ya jamii ni Msingi imara wa uwezeshwaji wananchi.
Dkt.John ameeleza kuwa jukumu walilonalo kitaifa nj kufanya maendeleo ya jamii katika wakati uliopo na kuhakikisha wanakuwa taasisi ambayo inasimamia jukumu hilo na kulipeleka katika wakati wa karne iliyopo sasa ya teknolojia na maendeleo ambayo yanakamilika kila siku.
"Kwa niaba ya taasisi ningeomba tutumie siku hizi mbili za kongamano vizuri sana tujadiliane kwa uwazi ,tuelezane na baada ya hapa mimi mwenyewe nitakuja ofisini kwako kukuambia jambo ambalo linatija."Alisema Dkt.John Lusingu
0 Comments