SERIKALI YAWEKEZA AGENDA YA KITAIFA YA AFYA YA MAENDELEO YA VIJANA BALEHE KWA VIJANA NCHINI - Matukio Daima Media

Latest

Kwa Habari za kitaifa, Habari ya Kimataifa! Habari za Michezo, Burudani na habari za mataifa mbalimbali usiache kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii kama Facebook, Instagram, YouTube, Twitter, Tiktok, na Threads. Matukio Daima, Ni yetu Sote!



MAGAZETI

KARIBU MIDLAND HOTEL, DODOMA

Legacy Academy Schools

Hanezye Schools

Hanezye Schools

Tuesday, November 21, 2023

SERIKALI YAWEKEZA AGENDA YA KITAIFA YA AFYA YA MAENDELEO YA VIJANA BALEHE KWA VIJANA NCHINI

 




Na, Jusline Marco: Arusha


Waziri wa maendeleo ya jamii, Jinsia, wanawake na makundi maalumu Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema serikali kwa kutambua mchango wa vijana nchini imeamua kuwekeza agenda ya kitaifa ya kuwekeza katika afya na maendeleo ya vijana balehe nchini.


Dkt. Gwajima ameyasema hayo Jijini Arusha wakati akifungua Kongamano la 16 la Wataalamu wa maendeleo ya jamii na Maadhimisho ya  miaka 60 ya Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru, amesema asilimia kubwa katika taifa ni vijana balehe kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.


Ameongeza kuwa mpango wa kuwekeza kwenye maendeleo na afya kwa vijana balehe ulizinduliwa mwaka 2021/22 hadi 2024/25 ambapo agenda hiyo imejikita katika kutengeneza nguzo kuu sita ambazo ni kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kutokomeza mimba za utotoni, kuzuia ukatili wa kimwili kwa watoto, wanawake na wanaume, kuboresha lishe, masuala ya kisaikolojia, kuhakikisha watoto wakike na wakiume wanabaki shuleni pamoja na kuwajengea vijana balehe ujuzi na uwezo wa kumfikia fursa za kiuchumi.

No comments:

Post a Comment