Header Ads Widget

RC DENDEGO ATANGAZA OPARESHENI ONDOA WAFANYABIASHARA HOLELA MJI MZIMA WA IRINGA


MKUU wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego ametangaza kuanza kwa Oparesheni endelevu ya safisha mji wa Iringa iliyopewa jina la Oparesheni ondoa wafanyabiashara Holela itakayoanza Novemba 19 mwaka huu.

Kupitia mkutano wa pamoja na wafanyabiashara Mjini Iringa uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa Mjini hapa Jana saa 12 asubuhi ,mkuu huyo wa mkoa alisema katika Oparesheni hiyo itashirikisha Vyombo Vya ulinzi na usalama ,Serikali ya mkoa ,Chama cha mapinduzi (CCM) mkoa , Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na wafanyabiashara wenyewe haita muacha mtu .

Hata hivyo alisema tayari wafanyabiashara ndogo ndogo Machinga wamekwisha pangwa maeneo Yao ila kimeibuka kikundi cha wafanyabiashara Holela ambacho kinafanyabiashara sehemu yeyote. Alisema jambo hilo halikubaliki na ni kinyume na utaratibu wa Sheria za mipango miji .

Hivyo alisema wote ambao wanafanyabiashara maeneo yasiyo rasmi kuanza kuondoka kwenda maeneo rasmi ama kuwasiliana na Viongozi wa Machinga ama Manispaa Ili Kupewa maeneo sahihi si vinginevyo .

Hivyo alisema Mkataba wa makubaliano pande zote umeandaliwa na tayari kutekelezwa . Dendego alisema toka mwezi wa tatu mwaka huu serikali imejaribu kuwapanga wafanyabiashara wadogo ndani ya mji ili kurahisisha ufanywaji wa biashara kwa urahisi na ufanisi.

Alisema wamefanya zoezi hilo katika mazingira magumu sana wakati wanaanza, kwani walifanya kwa Zaidi ya mara mbili na zote bado hawakupata matokeo Chanya, kwani kila wanapowapanga wafanyabiashara hawa wadogo  kwa kuwatoa katika maeneo ambayo wanaona ni hatarishi au waliyoyakataza, bado wamekuwa wakirudi katika maeneo hayo hayo na mbaya Zaidi wanaenda kuzuia watu wengine kufanya biashara.

Dendego alisema lengo la serikali ni kuhakikisha kila mdau afanyie biashara yake sehemu stahiki, kama wa sokoni ni sokoni na dukani ni dukani, kwani wote wanathamini, lakini kufanyia baishara barabarani au mbele ya biashara ya mwingine sio uungwana na wala sio sawaswa. =

"Na hili limekuwa likileta maumivu makubwa sana kwa wafanyabiashara wa maduka…’’

Alisema Oparesheni inayokwenda kufanyika Itakuwa ni mji mzima wa Iringa na haitakuwa mashine tatu pekee ama Miyombonj kama ilivyokuwa awali .

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Aliupongeza uongozi wa  Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Masoko ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa uvumilivu na ukomavu katika kulisimamia suala hilo .

alisema kuwa viongozi wa jumuiya hiyo wamekuwa wakiifikia serikali na kuwasilisha malalamiko yao na wamekuwa wakisikilizwa na wameshuhudia kwa namna gani serikali inapambana kuhakikisha vita hiyo inashinda kwa mstakabari wa maendeleo ya taifa kwa ujumla, kwani hii ni vita ya uchumi.

Mkuu huyo wa mkoa aliwaomba wakazi wa mkoa wa Iringa kushirikiana na viongozi wa serikali kuhakikisha masuala haya yanafanikiwa pasi kuwa na changamoto, kwa lengo lakufungua na kuzitumia fursa mbalimbali mkoani hapa.


"Nyinyi wenyewe ni mashahidi sisi viongozi wenu hatulali, kuhakikisha kila siku Iringa kuna shughuri zinaendelea kufanyika, watu waje wengi Iringa ili muweze kufanya biashara, nyinyi mashahidi hivi juzi tu tumetoka katika maadhimisho ya Utalii ya Karibu Kusini, tulikuwa na wageni wengi sana hapa Iringa, na kila aliyefanya biashara aliuza, tumetoka Karibu kusini tumewaletea SHIMIWI Taifa  hapa na Zaidi ya watu elfu tatu walikuwepo hapa, na hapa juzi kulikuwa na mashindano ya magari ya afrika, ASAS RALLY OF AFRIKA, kwa hiyo kila mfanyabisahara aliitumia hiyo fursa na sisi serikali kazi yetu ni kuwaletea nyinyi wateja..’’

 Dendego alisema wataanza oparesheni maalumu Novemba 19 mwaka huu itakuwa ya kwanza na ya mwisho na hivyo kuwataka  kila mfanyabiashara arudi kwenye eneo lake na kwa wasio kuwa na eneo basi wafike kwa mkurugenzi na atapangiwa. 

Mwanasheria wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Nicholaus Mwakasungura akisoma Hati hiyo ya makubaliano alifafanua umuhimu wa wafanyabiashara kufuata taratibu zinazotakiwa ili kuepusha changamoto zozote, na hati hiyo ni kama ifuatavyo. Alisema hati ya maridhiano ni kati ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa,uongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Iringa,Umoja wa wafanyabiashara WA masoko na uongozi wa Machinga Iringa ambayo ni hati ya uthibiti wa wafanyabiashara Holela .


 Alisema hati hiyo Alisema alisema Kwa kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imejenga masoko katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri,Kwa kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ina nia ya kuwaondoa wafanyabiashara wote holela wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.

Aidha alisema Kwa kuwa Jumuiya ya wafanyabiashara wanahitaji maeneo wanayofanyia biashara kuwa masafi ,Kwa kuwa Umoja wa Wafanyabiashara wa Masoko wanahitaji maeneo ya masoko yawe safi. Alisema Kwa kuwa Shirikisho la Wamachinga Wilaya ya Iringa wanahitaji wafanyabiashara holela wahamie kwenye maeneo yaliyo rasmi kwa biashara;Hivyo basi, maridhiano haya yanashuhudia haya yafuatayo

Kwanza  Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Tanzania, Umoja wa Wafanyabiashara wa Masoko na Shirikisho la Wamachinga Wilaya ya Iringa watafanya operesheni ya safisha mji yenye kaulimbiu "Iringa uchafu sasa basi".

Pili  zoezi hili la safisha mji linakusudiwa kufanywa kwa pamoja na wadau wote wa usafi katika Halmashauri na viunga vyake.

Sehemu ya tatu ni  Kwamba zoezi la usafi litakuwa endelevu likiwahusisha wadau wa maridhiano haya wakati makubaliano ya nne ni Kwamba wadau wa maridhiano haya kwa pamoja wameridhia kuwa operesheni safisha mji itaanza tarehe 20/11/2023.5. Kwamba tarehe 19/11/2023 ni hatua za awali zitakazofanywa kwa pamoja ikiwahusisha Mkuu wa Mkoa pamoja na kamati yake ya usalama Mkoa,  Mkuu wa Wilaya ya Iringa pamoja na kamati yake ya usalama Wilaya, viongozi wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya Mkoa na Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Wataalam wake, viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Viongozi wa Umoja wa Wafanyabiashara masokoni, viongozi wa Shirikisho la Machinga Wilaya ya Iringa kwa pamoja watapita kuwajulisha wafanyabiashara holela kuondoka maeneo yasiyo rasmi pasipo shuruti na kuhamia sehemu rasmi.

Sehemu ya sita ni Kwamba maeneo yatakayo husika na operesheni safisha mji ni pamoja na maeneo yote ya vichochoro vilivyozibwa na wafanyabishara hao holela, mifereji na Barabara za mji, maeneo ya masoko, maeneo yote ya wazi, maeneo ya stendi, maeneo ya kutolea huduma kama vile hospitalini na Magereza.  Wakati sehemu ya Saba  Kwamba zoezi la safisha mji litafanyika eneo la Mashinetatu, Miyomboni, Magari mabovu, Mlandege, Ipogolo, Zizi, Kihesa na kwingineko itakapoonekana itafaa.

Alisema sehemu ya Nane ya maridhiano hayo ni Kwamba hakuna upande wowote utakaokwenda kinyume na maridhiano haya

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI