Diwani wa kata ya Mirongo Hamidu Said ameeleza kuwa amepatwa na sintofahamu ya jina lake kukatwa katika nafasi ya naibu meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza baada ya uchaguzi kufanyika na yeye kupata ushindi wa kura 14 huku mpinzani wake akiwa na 10.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa uchaguzi uliofanyika juni 21 mwaka huu katika ukumbu wa ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana uliohudhuliwa na wajumbe 24 kati ya 26 na kinyang' anyiro hicho kuwa na wagonbea watatu, Bhiku Kotecha, Hamidu Said pamoja na Charles Nyamasiriri na yeye kuibuka kuwa mshindi.
Hamidu ameeleza kuwa baada ya kupata ushindi huo katika zoezi la kuthibitishwa na Baraza la madiwani kuwa Naibu Meya alishangazwa na kitendo Cha jina lake kukatwa bila kupewa taarifa Kwa nini jina lake limekatwa katika nafasi hiyo.
"Wamenirundikia vitu vingine sana mpaka sasa sijaelewa ni Kwa nini jina langu limekatwa, mapungufu yangu yote wanataka kunirundikia mimi hayo yako ndani ya Baraza kanuni na miongozo kama Mimi nina makosa basi yalipaswa kupelekwa kwenye baraza la madiwani kama Kuna utendaji unaonekana kwenda kinyume" Alisema Hamidu.
Ameeleza kuwa Kuna baadhi ya watu wanabeba mambo ya Serikali kupitia Mgongo wa chama ili kuweza kumuumiza na kushindwa kumtendea haki wakati Kila jambo linalozungumziwa liko wazi.
"Kanuni zetu ni Kali sana kama kuna mambo ambayo nimefanya kinyume ilipaswa nichukuliwe hatua za kinidhamu ndani ya baraza" Alisema Hamidu.





0 Comments