Header Ads Widget

ZAIDI YA NYUMBA 22 NACHINGWEA ZIMEBOMOKA KUTOKANA NA UPEPO MKALI NA MVUA KUBWA

ZAIDI ya Nyumba 22 katika Kijiji cha Nang'olola kata ya Stesheni wilaya ya Nachingwea zimeharibika kutokana na upepo mkali na mvua kubwa zilizonyesha siku ya Jana na kusababisha wananchi kukosa makazi na chakula.


Wakizungumza wakati walipotembelewa na viongozi wa serikali ya wilaya ya Nachingwea, wananchi hao walisema kuwa wamekosa mahali pa kukaa na chakula kutokana na kuharibiwa na mvua kubwa pamoja na upepo mkali uliotokea siku ya Jana katika Kijiji hicho.



Wananchi hao walisema kuwa wanaiomba serikali kuwatatulia tatizo la makazi pamoja chakula kutokana na changamoto ambazo wamekumbana nazo.

Wananchi walisema kuwa wanamshukuru mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo sambamba na Kamati ya maafa Kwa kuwatembelea na kuwafariji Kwa kile kilichotokea. 


 Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka wananchi kuwa na utulivu wakati serikali ya wilaya Nachingwea ikiwa inafanya jitihada ya kuwanusuru na janga hilo. 

Moyo ameongeza kwa kusema kuwa wananchi wachukue tahadhari Katika kipindi hiki cha masika na mvua za elinino Kwa kuhama Katika maeneo ya mabondeni. 


Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Mhandisi Chionda kawawa amesema kuwa wanafanya tathimini ili waweze kuchukua hatua haraka.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI