Header Ads Widget

NGAJILO AKICHANGISHIA CHUO CHA RUCU MILIONI 59

 


MWENYEKITI wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Fadhili Ngajilo amekifanikishia fedha za Ujenzi wa Chuo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ruaha Catholic University (RUCU) kiasi cha Tsh  milioni 59.

Ngajilo amechangisha fedha hizo katika Hafla ya harambee iliyofanyika Jumamosi Oktoba 28 mwaka huu katika  ukumbi wa Rev. Dr. Cephas Mgimwa ndani ya campas ya RUCU.

Hafla hii ya uchangiaji imefanyika ukumbi wa Rev. Dr. Cephas Mgimwa ndani ya campas ya RUCU.

 Kiasi hicho cha Tsh milioni 59 ni  kati ya hitaji la Shilingi  milioni 270 zinazohitajika kumalizia ujenzi na kuweka vifaa vya mafunzo kwa mazoezi. 


Pamoja na kuwashukuru wachangiaji wote Ngajilo alimuomba makamu mkuu wa Chuo Rev. Prof. Pius Mgeni iandaliwe hafla nyingine ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuiinua sekta ya afya nchini na hususani mkoa wa Iringa.

Chuo cha RUCU tayari kimesajiri wanafunzi 400 mwaka huu 2023 kati ya 1,000 ya walioomba fani ya ufamasia.

Hivyo kutokana na wingi wa wanafunzi imebidi juhudi zifanyike kuwaunganisha wadau kukichangia chuo hicho kiweze kutoa huduma kwa ufanisi. 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI