Header Ads Widget

NAIBU KATIBU MKUU UVCCM BARA AIPA TANO MICHUANO YA SAMIA CUP JIMBO LA SAME MASHARIKI.



NA WILLIUM PAUL, SAME.

 


NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Bara, Mussa Mwakitinya (MNEC), amesema kuwa, mashindano ya Samia cup yaliyozinduliwa Jimbo la Same mashariki yatasaidia kuibua vipaji vya vijana watakaopata ajira katika klabu mbalimbali hapa nchini.

 

Naibu Katibu Mkuu huyo, alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua mashindano hayo ambapo alisema kuwa, mashindano hayo ambayo yatahusisha timu zipatazo 91 yal;iyofadhiliwa na Mbunge wa Jimbo la Same mashariki yanapaswa kuigwa na wabunge wotye nchini kwani yanaidia kuibua vipaji lakini kuwakutanisha vijana pamoja na kubadilisha mawazo ili kujiletea Maendeleo.

 


“Mashindano haya ni muhimu sana katika jamii kwani michezo ni ajira na yatasaidia vijana kuibua vipaji lakini pia kujenga afya zao na pia itasaidia kujiepusha na magonjwa ambukizi pamoja na kuingia katika vitendo vya jinai” alisema Mnec Mwakitinya.

 

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kuwa, pia michezo ni fursa kwa Serikali kueleza yale yote yaliyofanywa kwa wananchi na kutambua nini ambacho Serikali imefanya na inachodhamiria kufanya mbeleni hivyo Mbunge Anne Kilango ameonyesha mfano bora na kuamua kuyapa mashindano hayo jina la Rais Samia lengo ni kumshukuru kwa jinsi ambavyo ametoa fedha nyingi zaidi ya Bilioni 9 katika miradi ya Maendeleo jimbo la Same mashariki.



Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana kuhakikisha wanawalinda watoto wa kike ili kuweza kutimiza ndoto zao za badae.

 

Kasilda alisema kuwa ni jukumu la kila kijana kuhakikisha wanawalinda watoto wa kike waweze kufikia ndoto zao za badae pamoja na kuwaibua wale wote wenyenia hofu ya kuwakatisha watoto shule kwa kuwarubuni ili waweze kuchukuliwa hatua.

 


Naye Katibu wa Mbunge Anne Kilango Malecela, Semu Mmamba alisema kuwa, mashindano hayo yanayofadhiliwa na Mbunge yanalengo la kutangaza kazi zilizofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani katika jimbo la Same mashariki pamoja na kumshukuru pamoja na kutekeleza Ilani ya uchaguzi.

 


Pia yatasaidia kuibua vipaji vya vijana katika michezo na kuwatengenezea mazingira ya kujitengenezea ajira katika michezo pamoja na kuwaunganisha wananchi hususani vijana na kuwaepusha na vitendo visivyokubalika katika jamii.

 

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI