Header Ads Widget

NAIBU KATIBU MKUU MWAKITINYA "VYAMA VYA UPINZANI VINAENDA KUKISINDIKIZA CCM UCHAGUZI MKUU 2025"



NA WILLIUM PAUL, SAME.

 

NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Bara, Mussa Mwakitinya (MNEC), amesema kuwa kazi kubwa ambazo zimefanywa na Serikali ya awamu ya sita kupitia Ilani ya uchaguzi 2020/2025, vyama vya upinzani vinaenda kukisindikiza chama cha Mapinduzi kushika dola katika uchaguzi mkuu 2025.

 

Mnec Mwakitinya alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na Wananchi wa Jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro waliojitokeza kwa wingi katika kata ya Mpinji kushuhudia ufunguzi wa mashindano ya Samia cup.

 


Alisema kuwa, Serikali ya awamu ya sita imeweza kujidadavua kwa wananchi kwa kufanya mambo makubwa katika sekta mbalimbali ambapo imeweza kutekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi hali ambayo itasaidia Chama cha Mapinduzi kutotumia nguvu kubwa kuwashawishi wananchi kwani kazi zenyewe zinajisema.


“Kutokana nkazi kubwa zilizofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani vyama vya siasa vya upinzani vitakwenda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kukisindikiza chama cha Mapinduzi tu na wala sio kushindana maana havina hoja za kuwaeleza wananchi kwani yale yote ambayo yalikuwa kilio cha wananchi Serikali ya awamu ya sita imeyatekeleza kwa vitendo” alisema Mnec Mwakitinya.



Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kuwa, katika jimbo la Same mashariki pekee tangu mwaka 2020 mpaka sasa serikali imeshatoa zaidi ya Bilioni 9.2 kwa ajili ya shughuli za miradi mbalimbali ya Maendeleo ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, Anne Kilango amekuwa akipambana kuhakikisha matatizo ya wananchi wake yanapatiwa ufumbuzi.

 

Alisema kuwa, Mbunge wa Jimbo hilo anatambua vizuri kazi yake ya kuwatumikia na kuwaletea Maendeleo ambapo amekuwa akimkumbusha Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani na Serikali kuendelea kutoa fedha mbalimbali kwa ajili ya shughuli za Maendeleo katika jimbo hilo.

 

“Wananchi wa Jimbo la Same mashariki hamkukosea kumchagua Anne Kilango Malecela na kura zenu hazijapotea kwani mbunge huyu amekuwa akipambana usiku na mchana kuhakikisha miradi mbalimbali ya Maendeleo inatekelezwa huku kwenu na anachokifanya anaungwa mkono na Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa kutoa fedha nyingi za Maendeleo” alisema Mwakitinya.

 

Alisema kuwa, kutokana na fedha nyingi zilizotolewa na Rais katika jimbo la Same mashariki, Wananchi hawana cha kumlipa zaidi ya kuombea na upendo pamoja na kuwapa kura za kishindo wagombea wtokana na chama chake cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani pamoja na uchaguzi mkuu 2025.

 

Aidha alisema kuwa, Chama cha Mapinduzi kinapambana kuleta Maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama wala dini na kudai kuwa hiyo ndio misingi ya CCM ni kitaendelea kufanya hivyo milele yote.

 

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI