Header Ads Widget

KUNENGE AISHUKURU SERIKALI FEDHA MIRADI YA MAENDELEO.



SERIKALI Kuu imeupatia Mkoa wa Pwani kiasi cha shilingi  trilioni 1.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo iliainishwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Hayo yalisemwa na Kamisaa ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge  wakati akiwasilisha taarifa ya miradi iliyotekelezwa mkoani humo katika kipindi cha Machi 2021 hadi Juni 2023 kwenye kikao cha Kamati kuu ya Chama hicho mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kwa Mfipa wilayani Kibaha.


Kunenge alisema utekelezaji wa miradi hiyo ni mafanikio makubwa yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya utawala wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambayo imetoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, nishati, maji na miundombinu ya barabara.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao alisema chama kimeridhika na miradi  iliyotekelezwa na serikali imetimiza  matakwa yaliyopo kwenye Ilani ya CCM  katika kuwaletea  maendeleo wananchi wake.


Kwa upande wake Katibu  wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani  Benard Ghatty alisema hadi sasa serikali imefikisha asilimia 98 ya  utekelezaji wa miradi na kwamba sehemu iliyosalia ni ndogo ambapo wanaamini ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu miradi yote itakamilika.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI