Na Pamela Mollel,Arusha
Serikali imeitaka jamii kuhakikisha kuwa wanalinda mazingira ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha watoto namna ya kutunza mazingira ili kukabaliana na mabadiliko ya Tabia nchi
Kwa sasa mabadiliko ya tabia ya nchi hapa nchini yamesababisha kuwepo kwa madhara ambayo yanawakumba hata watoto jambo ambalo sasa watoto nao wanatakiwa kuanza kuchukua hatua ili kulinda kizazi kijacho.
Hayo yameelezwa jana Arusha na Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Raisi muungano na Mazingira,Sulemani Jaffo wakati akiongea kwenye siku ya watoto duniani ambayo kwa Tanzania imeazimishwa Arusha.
Jaffo alisema kuwa siku ya mtoto ni muhimu sana hasa kwenye suala zima la mazingira ambapo kwa sasa bado madhara ya mabadiliko ya tabia ya nchi yameendelea kuathiri jamii hasa watoto.
Alidai kuwa mabadiliko hayo ya tabia ya nchi yanaweza kuepukika endapo tu jamii itaungana kwa pamoja lakini pia kuwahusisha watoto kwa kuwa hata nao yana waathiri sana.
"mjengee mtoto kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi hii itamfanya aweze kuwa balozi mzuri wa mazingira na hata athari zitapungua kwa kiwango kikubwa kwani zina waathiri hata wao"aliongeza.
Alimalizia kwa kusema kuwa Serikali imejiwekeza katika kumsaidia mtoto kwani mtoto ana haki ya kuthaminiwa pamoja na kuendelezwa.
Naye Naibu Katibu mkuu Wizara ya maendeleo ya jamii Amon Mpandu alisema kuwa watoto wana haki zao jamii inatakiwa ihakikishe kuwa zinafuatwa.
Alisema haki za watoto kama vile haki ya kuishi, haki ya kulindwa dhidi ya mambo yahusuyo ukatili, kuendelezwa kielimu,pamoja na kushirikishwa katika mambo mbalimbali yahusuyo Jamii.
Awali watoto ambao walishiriki katika siku hiyo walisema kuwa pamoja na kuwa haki zao zinalindwa kwa kiwango kikubwa sana lakini jitiada kubwa dhidi ya mabadiliko tabia nchi, Kwa watoto zinaitajika kwa haraka
Watoto hao walidai kuwa wapo baadhi ya watoto ambao wanaongoza kwa kuharibu mazingira kwa kuwa hawana elimu thabiti ya mazingira hivyo ni muhimu kwa kila mzazi kuhakikisha anakuwa balozi ikiwezekana kila mtoto kupewa mti na sehemu ya kutunza ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kwa upande wake mkurugenzi mkaazi wa shirika la watoto Duniani UNICEF Elke Wisch amesema watoto hawapaswi kuachwa nyuma kwenye mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwani wakiwezeshwa kuwa na kizazi kinachotunza na kuyalinda mazingira
Maadhimisho ya siku ya watoto Duniani ni kumbukizi ya azimio la umoja wa mataifa juu ya haki za watoto lililofanyika mwaka 1989 na nchi wanachama walikubaliana kufanya maadhimisho hayo kila ifikapo November 20 kila mwaka.
0 Comments