Header Ads Widget

KOROSHO IKIDONDOKA IOKOTWE HARAKA KABLA HAIJAINGILIWA NA UNYEVU - MNG'ERESA

 




Na Scolastica Msewa, Mkuranga


Mwenyekiti wa Chama kikuu Cha Ushirika wa Wakulima wa Mkoa wa Pwani CORECU Musa Mng'eresa amewataka Wakulima mkoani humo kuendelea kulinda ubora wa korosho zao kwa kuokota Korosho kila siku ili zibaki kwenye ubora stahiki hasa ni kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha nchini kote.


Akihutubia katika mnada wa pili wa korosho uliofanyika katika ghala kuu la Wilaya ya Mkuranga huko Kijiji cha Kingoma Mng'eresa amesema  Korosho zikidondoka mtini isilale shambani haraka ziokotwe ikahifadhiwe vizuri ili kulinda ubora wake.


Amesema mvua kwenye Korosho ni changamoto kubwa ingawa Wakulima wanaendea kuzianika Korosho zao ili kuondoa unyevu ambao uathiri ubora wa korosho mkoani Pwani. 



"Korosho ikidondoka haitakiwi kulala ardhini na iwapo italala shambani hapo bila kuokotwa itaingiliwa na unyevu ambao hupelekea kupunguza ubora wa korosho ya mkulima hivyo tuokote Korosho zetu mara kwa mara.


Akizungumzia maandalizi ya kilimo cha zao la mbaazi ambalo ni zao jipya la biashara mkoani humo Mng'eresa amesema tayari wamenunua Tani 3 za mbegu za mbaazi ambazo zipo hatua za mwisho za ugawaji kwa wakulima.


"Wakulima msiwe na hofu tayari tumeshanunua mbegu za mbaazi mtagawiwa hivi karibuni"

Meneja wa Chama kikuu Cha Ushirika wa Wakulima wa Mkoa wa Pwani CORECU Mantawela Hamisi akitoa taarifa kwenye mnada wa pili ulifanyika November 15 mwaka huu amesema Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimeathiri uuzaji wa zao la Korosho mkoani Pwani ambapo Tani zaidi ya 1500 zilishindwa kuuzwa katika mnada wa pili wa November 8 mwaka huu kutokana na zao hilo kuingiwa na unyevu ambao ni hatari kwa zao hilo.


Amesema Korosho hizo Tani zaidi ya 1500 zimeunganishwa kwenye Tani 3187 zilizouzwa kwenye mnada huu ambapo bei ya wastani wa shilingi 1809.46 kwa kilo moja.


Amesema athari ya mvua ni kubwa lakini lengo la mkoa wa Pwani ni kuuza Korosho zenye ubora hivyo tunahimiza Wakulima kuendelea kuanika Korosho zao kila jua linapowaka hadi zitakapokauka.

 

Wakulima bado wana Korosho nyingi majumbani wakiendelea kukausha kuondoa unyevu hivyo zinavyokauka watapeleka kwenye vyama vya msingi ili zipelekwa kwenye maghala ya Chama kikuu CORECU tayari kwa kuuzwa.


Mkulima wa korosho Sultani Juma ameshukuru kwaajili ya bei nzuri ya Korosho katika minada hiyo ukilinganisha na hali ya hewa ya mvua na kusema mvua inanyesha kwa wingi, hivyo uwezo wa kuzihifadhi na kuzikausha ni kazi ngumu.





++++++++++++++

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI