Header Ads Widget

RUFAA YA MJANE WA NYAMA YA SWALA YAFIKIA PAZURI

 


JOPO la Mawakili 10 kutoka chama cha mawakili Tanganyika (TLS) pamoja na mwanasheria wa Umoja wa  wanawake Tanzania (UWT) Taifa wamekamilisha usajili wa rufaa ya mjane Maria Ngoda aliyefungwa jela miaka 22 kwa kosa la kukutwa na vipande 12 vya nyama ya Swala kinyume na Sheria.


Wakili wa TLS Moses Ambindwile akizungumza matukio Daima Media  mahakamani hapo Jana   alisema kuwa zoezi la usajili wa Kesi hiyo umekamilika Novemba 14 saa 7 mchana 


Alisema kuwa kimsingi usajili wa awali ulifanyika Novemba 13 majira ya jioni  walikuwa wamesajili ila kutokana na changamoto za mfumo wa Kieletronikia uitwao Electronic Case  System (eCMS) Kesi hiyo  walikwama kupata namba ya usajili wa Kesi hiyo .



Hivyo kulazimika kufanya mchamato upya wa usajili wa Kesi hiyo hiyo ambao Sasa wamefanikiwa kusajili na kupata namba ya Kesi hiyo.


"siku ya tarehe 14 November 2023  majira ya mchana  Rufaa ya Maria Ngoda ilifanikiwa kuingizwa katika mfumo mpya wa kusajiri  mashauri kwa njia  ya  kielektronikia uitwao ELECTRONIC CASE MANAGEMENT SYSTEM (eCMS)  hatua inayofuatia ni upande wa Mahakama kuisajiri Rufaa hiyo na kutoa summons kwa ajili ya hatua ya usikilizwaji" alisema Wakili Ambindwile


Wakili Ambindwile ambae alikuwa ameongoza na Wakili Mchungaji Joshua Chusi na mwanasheria wa UWT  Abdul Marijan alisema kuwa namba ya usajili (Admission) ni  84101 /2023 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa .


Mbali ya Wakili Mchungaji Chusi ambae ni Mwenyekiti wa dawati la msaada wa kisheria katika Ofisi za TLS Iringa aliwataja mawakili wafuatao panda mahakamani kumtetea mjane huyo katika rufaa hiyo kuwa   Dr. Rwezaula Kaijage, Frank Ngafumika,  Barnabas Nyalusi, Jane Massey, Samson Rutebuka, Wakili Mchungaji  Joshua Chusi,Innocent Kibadu, Cosmas Kishamawe na Jali Mongo pamoja na yeye mwenyewe ambae atakuwa muongozaji wa Jopo hilo la mawakili huku mwanasheria wa UWT akiwasaidia kufanya tafiti .


Hata hivyo alitoa wito kwa mawakili wengine wanaohitaji kuongeza Nguvu zaidi kwenye rufaa hiyo ruksa kujitokeza .


Wakili Andimbwile alisema baada ya kuwa wamesajili Kesi hiyo Sasa wanasubiri  mahakamani ipange jaji wa kusikiliza Kesi hiyo japo alisema mara baada ya kupanga jaji   hukumu kutolewa ni ndani ya siku 45.


Alisema mfumo wa usajili wa Kesi Kieletronikia uitwao Electronic Case System ( eCMS) ni mfumo mzuri ulianza Novemba 6 mwaka huu ila unachangamoto zake hasa mtandao unaposumbua huwezi kusajili online na kupata namba ya Kesi .


 Katika hatua nyingine Wakili Ambindwile alisema pamoja na kuwa hukumu ya mjane huyo imekuwa ikifuatilia sana na Jamii Bado ameitaka jamii na umma wa watanzania, ambayo imeguswa kihisia,  kuwa na utulivu kwani jambo hilo la kisheria na mahakama nj chombo cha kutafsiri Sheria hivyo ni imani yao haki itatendeka.


Kwa upande wake naibu msajili wa mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa Malewo Maximillian alipofuatwa na mwandishi wa habari hiyo Ili kujua kama Kesi hiyo imesajiliwa alisema ni kweli Kesi hiyo imekwisha sajili na kinachoendelea Sasa ni upande wa mahakama kupanga jaji wa kusikiliza .


 Hukumu dhidi ya Maria Ngoda ilitolewa Novemba 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha  kuwa ni kweli mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000 kinyume na Sheria .


Akitoa hukumu hiyo kwa mjane huyo mkazi wa Zizi la Ng’ombe mjini Iringa, Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, Mkasiwa alisema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 86 (1) (2) (c) cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba tano ya mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho na kifungu cha 59 (a) (b) cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2016.


Wakati akijitetea bila usaidizi wa wakili  mjane huyo alikiri ni kweli alikutwa na ndoo yenye nyama hiyo ambayo alidai alikabidhiwa na mtu aliyemtambua kwa jina moja la Fute bila kujua ina nyama ya nini .


Alisema alilazimishwa abebe ndoo hiyo na kufikishwa kituoni na kufunguliwa kesi ya kukutwa na nyara za serikali sambamba na kosa la uhujumu uchumi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI