Na Gift Mongi MATUKIODAIMA SONGEA
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Fakii Raphael Lulandala (Mnec) ametembelea Vijana NEW DESTINY GROUP wanufaika wa Mikopo (4%) ya Halmashauri ya wilaya ya Songea Mjini na kujifunza mengi kutoka kwao.
NEW DESTINY GROUP ni kiwanda cha Vijana kinachochishughulisha na utengenezaji wa mifuko (Vifungashio).
Aidha vijana hao walipata mkopo wa kiasi cha Tshs. Million 192 huku Mashine zikiwa na Thamani ya Million 120 na jengo likiwa na Thamani ya Million 50 na kiasi kilichobaki wamenunulia malighafi za uzalishaji.
Vijana wa NEW DESTINY GROUP wameishukuru Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu HassanRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa fursa hii ya kuwawezesha vijana mitaji ya uwekezaji na ujasiriamali kwani imewakwamua kiuchumi.
Sambamba na hilo Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa ameelekeza kwa niaba ya Mwenyekiti wa UVCCM Mohammed Ali Kawaida (MCC)* Halmshauri zote nchini kujifunza kutoka Halmashauri ya Songea Mjini kwa kutenga maeneo (ardhi) kwa ajili ya Uwezeshaji na Uwekezaji kwa Vijana.
Miongoni mwa vijana hao Deodatus Mkilinya amesema upatikanaji wa fedha za mikopo zimekuwa na faraja kubwa katika kuwainua vijana kiuchumi.
'Tunaishukuru serikali Kwa namna wanavyotukwamua vijana na kutuwezesha kujiajiri badala ya kuishi Kwa kusubiria kuajiriwa pekee'amesema
0 Comments