Leonida Mushama Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa Kigoma
xxxxxx
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa Kigoma (TAKUKURU) imesema kuwa kuna upunguzi mkubwa umegunduliwa kwenye jumla ya miradi 33 yenye thamani ya shiligi Bilioni 12.5 iliyofuatiliwa na taasisi hiyo ikionyesha kuwa chini ya kiwango.
Mkuu wa dawati la elimu kwa umma mkoa Kigoma,Leonida Mushama alisema hayo akitoa taarifa ya utekelezaji ya taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu Julai hadi Septemba mwaka huu kwa niaba ya Mkuu wa TAKUKURU mkoa Kigoma, Stephen Mafipa.
Mushama alisema kuwa katika miradi hiyo ipo pia miradi ya ujenzi wa madarasa inayotekelezwa kwa mpango wa BOOST yenye thamani ya jumla ya shilingi Bilioni tatu ambapo kumeonekana kuwepo kwa mapungufu kwenye ununuzi wa mabati yenye thamani ya shilingi Milioni 241.3 katika halmashauri ya Mji wa Kasulu na Halmashauri ya wilaya Kasulu.
Tayari TAKUKURU imeanzisha uchunguzi kwa ajili ya kuchukua hatua kwa watumishi wa halmashauri ya mji Kasulu na Halmashauri ya wilaya Kasulu waliohusika na kadhia hiyo kwa kutaka kufanya ubadhirifu kwenye miradi hiyo ya ujenzi wa madarasa kwenye shule hizo kupitia mpango wa BOOST.
Katika hatua ya awali Mushama alisema kuwa Mzabuni wa kampuni ya Kiboko katika halmashauri ya wilaya Kasulu aliwasilisha mabati mengine yenye viwango yenye thamani ya shilingi milioni 129 wakati Yule wa kampuni ya HERICON katika halmashauri ya mji wa Kasulu alirudisha fedha.
Alisema Mushama kuwa hali hiyo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na wataalam wa halmashauri kuwa na watu wao kwa ajili ya kununua vifaa vya ujenzi ambao huelekeza kamati za ujenzi na usimamizi wa miradi kwenda kununua vifaa kwa watu hao kwa ajili ya maslahi binafsi ya wataalam hao wa Halmashauri.
Miradi mingine iliyochunguzwa na TAKUKURU ni pamoja na ujenzi wa madarasa saba yenye thamani ya shilingi milioni 195.2 wilayani Kakonko, ujenzi wa shule mpya ya Msingi Kazilamihunda wilaya ya Kakonko wenye thamani ya shilingi milioni 361.5 na.
Aidha miradi mingine iliyochunguzwa na kukutwa na mapungufu ni ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 22 ya vyoo shule ya msingi Mahembe na ukarabati wa nyumba tano za walimu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 180.
0 Comments