Header Ads Widget

AJALI YA MAGARI MANNE NJOMBE YASABABISHA VIFO NA MAJERUHI






Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Magari manne yamepata ajali katika eneo la Ichunilo Ruhuji mjini Njombe na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine nane kujeruhiwa.


Kituo hiki kimefika katika eneo la ajali hiyo na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda akiwemo Emmanuel Mgaya, Jescar Madembwe na Geofrey Kabelege ambaye ni dereva wa basi la Kalubandika ambalo nalo lilikumbwa na mkasa wa Lori la mchanga wamesema eneo hilo limekuwa tatizo kwa vyombo vingi vya moto huku wakitoa wito kwa serikali kulitupia jicho la karibu.

Bahati Mkutani Mkaguzi wa jeshi la zimamoto na uokoaji na kaimu kamanda wa zimamoto mkoa wa Njombe


Mkaguzi wa jeshi la zimamoto na uokoaji ambaye ni kaimu Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Njombe Bahati Mkutani amesema baada ya kupokea simu ya ajali hiyo majira ya saa tatu asubuhi walikuta ajali ya gari moja kubwa lililobeba saruji baadaye likatokea lori la mchanga ambali lilifeli breki na kuanza kusababisha ajali ya watu wengine na magari mengine.

Dokta Hellen Msese mganga mfawidhi Hospitali ya mji wa Njombe Kibena


Miili na majeruhiwa hao walipelekwa katika Hospitali ya mji wa Njombe kibena ambapo Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dokta Hellen Msese amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi lakini hakuna aliyekuwa ametambulika.


Ezekiel Msalilwa na Theofonia Mligo ni majeruhi waliokutwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya mji wa Njombe Kibena ambao wamesema wamekutwa na ajali wakiwa katika eneo la tukio na wengine wakiwa wanaendelea kushuhudia.


Wito umeendelea kutolewa kwa madereva kuwa makini pindi wanapoendesha vyombo vyao vya moto hasa katika eneo hilo lenye mteremko mrefu na mkali unaotokea Kibena ambao umekuwa ukigharimu maisha ya watanzania wengi.

Baadhi ya majeruhi wakiwa katika Hospitali ya mji wa Njombe Kibena




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI