Na fatma Ally, Matukio DaimaApp.
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imeandaa matembezi ya Amani yatakayofanyika Desemba 2 Mwaka huu Jijini Dar es Salaam lengo ikiwa ni kudumisha amani na mshikamano nchini humo.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Machifu Tanzania Antonia Sangalali amesema kuwa matembezi hayo yatahudhuriwa na Rais mstaafu wa Jamuhuribya Muungano wa Tanzania ambapo mgeni radmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim.
Aidha, amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika matembezi hayo kwani lengo ni kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika kudumisha amani, hivyo ni vyema wananchi kushiriki.
Amesema kuwa, lengo la matembezi hayo ni kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuongoza kwa Amani na utulivu.
Ameongeza kuwa, Nchi bila Amani hakuna chochote kinachoweza kufanyika Kwamba Amani ni kitu muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote lile.
Ametumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyeki wa JMAT Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salam kwa ubunifu wake huo wa kuandaa matembezi hayo.
0 Comments