Header Ads Widget

HOJA YA MBUNGE KABATI YAFANYIWA KAZI ,KIKWETE AAGIZA VIJANA WALIOJITOLEA WAPEWE AJIRA

 


Naibu  Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwaajiri watendaji waliokuwa wakijitolea Katika nafasi zilizotangazwa hivi karibuni.

Kikwete ameyasema hayo baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati kuuliza ni kwa nini watendaji waliokuwa wakijitolea kufanya kazi za utumishi hawakupewa kipaumbele wakati wa mchakato wa ajira Mpya Za Halmashauri zilizotangazwa na badala yake wakaajiriwa watumishi wapya.

Katika hoja ya  Kabati Alisema kuwa Kitendo Cha kutowapa nafasi ya ajira vijana waliokuwa wakijitolea kitawavunja moyo Vijana wengine ambao wanafanya kazi ya kujitolea wakitegemea kuajiriwa pindi ajira zinapotangazwa.


"Ukiangalia Katika Halmashauri yetu Kulikuwa na Vijana zaidi ya 40 waliopita kwenye usaili lakini waliojiriwa ni watendaji 10 Tena ambao wao Wana watu ambao wamewashika Mkono mpaka kupata nafasi hizo, ila wale ambao walikuwa wakijitolea na wana sifa zote wamekosa nafasi hizo, Naomba sana  Naibu Waziri uliangalie hili" Alisema Mh Kabati 


Akijibu hoja hizo Mh. Ridhiwan Kikwete Amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kuwapigia simu vijana waliokuwa wakijitolea Katika nafasi hizo kabla ya Ijumaa na kuwapatia Ajira hao kwanza.


"Nikuagize Mkurugenzi uwatafute hao vijana ambao walikuwa na sifa ya kupata ajira waweze kuajiriwa kwa sababu walijitolea kwa moyo wakijua fika watapa ajira" Alisema Naibu Waziri Kikwete.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI