Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Alan Bukumbi
Leo 21/11/2022 akizungumza na vyombo vya Habari amesema, Kwa
ujumla hali ya Mkoa wa Iringa ni shwari, Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa katika
kuimarisha ulinzi na usalama linaendelea kufanya doria na misako mbalimbali
ilikubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu ambapo limefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa pamoja na vitu mbalimbali.
Katika
operesheni na misako iliyofanyika kuanzia Novemba 11, 2023 hadi Novemba 20,
mwaka huu, kwa kushirikiana na Askari wa uhifadhi pamoja na vyombo vingine vya
ulinzi na usalama tumefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa thelathini na nne
(34) kwa makosa mbalimbli kama vile kupatikana na silaha kinyume cha sheria,
kupatikana na nyara za serikali, kuingia hifadhini bila kibali, kupatikana na
sumu na kujihusisha na ujangili.
Aidha katika
Operesheni hiyo silaha kumi na moja (11) zimekamatwa, silaha aina ya Gobore 10
na silaha aina ya shortgun moja pamoja na Goroli sabini na saba (77), baruti
kiasi cha robo lita, silaha sita kati ya hizo zilitelekezwa na wamiliki ambapo
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
linaendelea kufanya uchunguzi kuwabaini wamiliki wa silaha hizo, silaha hizi
zimekuwa zikitumika katika uwindaji haranu na ujangili pamoja na matukio
mengine ya kihalifu.
Vitu vingine
vilivyokamatwa ni pikipiki mbili MC.326 CJK aina ya HAUJUE rangi nyekundu na
Pikipiki aina ya Fekoni chesisi namba LDAPAJOB8LGB02359 ambayo haina namba za
usajili zilizotumika katika kusafirisha nyara za serikali pamoja na vifaa
kama shoka moja kisu kimoja, vipande vitano vya nondo,msumeno mmoja, mikuki
sita, mapanga mawili, unga wa baruti, nyaya ishirini na saba (27). Watuhumiwa
wote waliolamatwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Vilevile novemba
17,2023, majira ya saa 02:00hrs huko maeneo ya kijiji cha Nyang'oro kata ya
nyang'oro tumefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aitwaye James Mtewele (40)
mkulima na mkazi wa kijiji cha Migoli akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya
bhangi ikiwa imehifadhiwa katika gunia moja la kilo mia moja akisafirisha
kutoka maeneo ya llula kwenda kijiji cha Migoli. Mtuhumiwa atafikishwa
mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Halikadhalika
tumemefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aitwaye Edger Mbalanzi ambaye
alitoroka mahakamani, aliyekuwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 22/2018 kosa
kupatikana na nyara za serikali Meno ya Tembo ambaye atatumikia kifungo chake
cha miaka Ishirini jela.
Katika hatua nyingine Kamishna Msaidizi
Mwandamizi na Kamanda wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Godwell Ole Meing’ataki, alifafanua
namna vijana wengi wanavyotumika katika biashara haramu hususani ujangiri. Pia
alieleza namna risasi za kisasa na za kienyeji zinavyotumika kuulia Wanyama, walizokamatwa
nazo watuhumiwa huku zingine zikitengenezwa na watu wanaotengeneza silaha
haramu kama vile bunduki aina ya short gun na Gobole ambazo nazo pia zilikamatwa katika
oparesheni hiyo .
‘’..Majangiri wamekuwa hawachagui silaha, Kama ambavyo tunaona kuna sime, panga, mundu, Nyaya na silaha nyinine nyingi za jadi ambazo hutumika katika shughuri zao hasa majira ya usiku ambapo hutumia tochi zenye mwanga mkali na hata mbwa pia. Lakini pia sumu inayotumika kuulia Wanyama mbalimbali ambapo hasa katika kipindi ambacho mtu Ruaha umekauka, majangiri huingia na kumwaga sumu hizo kwenye madimbwi mbalimbali na kuua Wanyama wadogo kwa wakubwa, na isivyo bahati nyama hizo huuzwa kwa watu, hivyo wananchi wanaopenda kula nyama za wanyamapori wanaombwa kuacha kwani ni hatari kwa afya zao..’’
Kamanda Uhifadhi aliongeza juu viungo vya
wanyama waliokutwa navyo majangiri katika oparesheni hiyo ni Pamoja na kucha za
Mhanga, Ngozi ya Sungura, Meno ya Tembo, Pamoja na Kakakuona ambao soko lao has
ani soko la nje ambako huko hununuliwa kwa matumizi mbali mbali, huku wakiacha
athari kubwa katika maeneo ya uhifadhi nchini.
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa linatoa wito kwa wananchi kuendelea kushrikiana na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, na wote wanaojihusisha na matukio hayo waache mara moja kwani jeshi la polisi pamoja na askari wa wanyama pori wamejipanga kuhakikisha uharifu wa aina zote unatokomezwa.
0 Comments