Header Ads Widget

BAJAJI 8 ZA WIZI ZAKAMATWA NJOMBE, 163 WATUHUMIWA

 

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Mahammoud Banga


Na Gabriel Kilamlya matukio DaimaAPP NJOMBE


Jeshi la Polisi mkoani Njombe limekamata  bajaji nane na watuhumiwa 163 wa makosa mbalimbali yakiwemo ya wizi, uvunjaji, mauaji na ubakaji katika kipindi cha miezi miwili.


Mbele ya vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahammoud Banga amesema pamoja na vyombo hivyo vya usafiri lakini kuna mali mbalimbali za wizi zilizokamatwa kutokana na ushirikiano mkubwa wa wananchi na Jeshi hilo.


Aidha Kamanda Banga amesema pia wamemkamata mtuhumiwa mmoja ambaye amekutwa na bunduki anayomiliki kinyume cha sheria.

Richard Luganga mwenyekiti wa umoja wa madereva bajaji mji wa Njombe


Richard Luganga ni mwenyekiti wa Umoja wa madereva Bajaji mjini Njombe ambaye anasema kutokana na wimbi la wizi wa bajaji hizo wamelazimika kupunguza muda wa kazi hasa majira ya usiku huku wakiliomba jeshi la polisi kuongeza ulinzi na doria za mara kwa mara katika maeneo mbalimbali.


Kwa upande wao baadhi ya madereva bajaji mjini Njombe akiwemo Geofrey Mwinuka na Johnson Chota wameomba viongozi wao kuendelea kushughulikia changamoto zinazosababisha kutokea kwa wizi kwani wanapata adha ya maeneo ya kuzihifadhi bajaji hizo.


Vyombo vya ulinzi na usalama vimeombwa kuendelea kuwasaidia katika kukomesha matukio ya wizi wa vyombo vyao vya moto kwani wanapata hasara kubwa pindi vinapoibiwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI