Header Ads Widget

 MHAGAMA AWATAKA WANAUME KUPIMA VVU

Na Hamida Ramadhani Matukio Daima  AAP Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Jenista Mhagama amewata wanaume kujitokeza kupima Virusi vya UKIMWI kwani imebainika wazi jinsia ya kiume wako nyuma kushiriki suala Zima la upimaji VVU na kwamba zoezi hilo liwe endelevu. Wito huo ameutoa leo jijini hapa wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya  UKIMWI Duniani 2023 ambapo kitaifa yanafanyika Desemba 1 Mkoani Morogoro.  

Waziri Mhagama amesema  wanaume wamekuwa wakiwategea wake au wenza wao na kusahau kuwa mwanaume anaweza kuwa na maambukizi ya UKIMWI na mkewe asiwe na maambukizi hayo 

"Nitoe hamasa kwa wanaume msitege kwenda kupima na msiwafanye wakezenu chambo kwenye suala zima la kucheki afya wote mnatakiwa kupima na kuzitambua hali zenu kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kufikia malengo ya kidunia na kuzifikia 95 tatu ifikapo 2030," Amesema Waziri Mhagama. 

Kati hatua nyingine amesema kundi la vijana kuanzia umri 15 mpaka 24 limekuwa likichangia maambukizi mapya ya UKIMWI kwa asilimia 40. Amesema hali hiyo ni mbaya na nguvu ya ziada inatakuwa kutumika ili kufanikisha na kuondoka katika athali zaidi kwa kushiriki kwenye majukwaa na midahalo mbalimbali yalioandaliwa kwenye maadhimisho hayo.

Kwa upande wake Dkt,Anath Ruebembera Meneja Mpango wa taifa wa kuthibiti UKIMWI,Wizara ya Afya amesema upatikanaji wa vipimo vya kupima VVU  vinapatikana kila mahali ikiwa ni pamoja na hospitali za serikali na sekta binafsi ambapo kwa sasa wameongeza  kipimo kingine cha kujipima mwenyewe baadae kwenda kuhakikisha kwenye vituo vya afya.

" Upatikanaji wa Kondom tatizo ni kwamba zikizambazwa huwa zinachukuliwa kwa muda ule ule na hivi sasa tutaweka utaratibu wa mtu wa kutokutumia kondom zaidi ya moja mwisho iwe kondom 3 ili kila mtanzania imfikie maana wengine wamekuwa  wakichukua na kwenda kuuza"Amesisitiza Dkt,Anath

Naye Makamu Mwenyekiti wa watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi VVU (NACOFA) Emanuel Reuben Msinga amesema kama taasisi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuwakusanya vijana kuanzia miaka 15 na kuendelea pamoja na vikundi vya kuhamasisha kwenye kata na wilaya ambapo ni mfano hai ndani ya miaka 3.

Hata hivyo katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. 

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI