TAMISEMI WAIPONGEZA SERIKALI YA NACHINGWEA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) imeupongeza uongozi wa wilaya ya Nachingwea kwa usimamizi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa ubora unatakiwa kwa mujibu wa miongozo ya serikali.
Akizungumza
wakati wa ziara ya siku moja katika Hospitali ya wilaya ya
Nachingwea,mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za mikoa na
serikali za mitaa(TAMISEMI)Denis Rondo alisema kuwa wameridhishwa na ubora wa
miradi yote iliyojengwa katika hospitali hiyo.
Rondo
alisema kuwa majengo yamejengwa kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya
fedha ambayo imetolewa na serikali kuu
au mapato ya ndani. Alisema kuwa kamati kwa ujumla inaupongeza uongozi wa
Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kwa kutumia mapato ya ndani kujenga hodi ya
maalumu ambayo itasaidia wagonjwa kulazwa kwenye hodi hiyo. Rondo alisema kuwa
kamati imejiridhisha kwa ubora unaotakiwa kwenye ICU ambayo imekuwa moja ya ICU
bora Tanzania kutokana na ubora wa jingo lake na vifaa tiba ambavyo serikli ya
awamu ya sita imepeleka katika ICU hiyo.
Awali
akitoa taarifa kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za mikoa na serikali za
mitaa (TAMISEMI),kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Nachingwea DR
Ramadhan Mahiga alisema kuwa hospitali ya Nachingwea ilipokea kiasi cha sh.
841,135,130 kwa ajili ya ujenzi wa jingo la OPD,maabara,jingo la
kufulia,kichomea taka na mtambo wake lengo likiwa ni kuboresha utoaji huduma
kwa wananchi wanaofika katika hospitali hiyo.
Mahiga
alisema kuwa wanaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kufanya
maboresho katika eneo la upatikanaji wa
bidhaa za afya(dawa na vifaa tiba) kupitia bohari ya dawa. Alisema kwa kipindi
cha julai 2021 hadi juni 2022 wilaya ilipokea fedha kiasi cha sh.
392,380,843.11 na kwa kipindi cha julai 2022 hadi juni 2023 wilaya ilipokea
fedha kiasi cha sh 705,638,762.92 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba
katika vituo vya kutolea huduma ya afya ambapo ni ongezeko la mara mbili
kupitia ruzuku
kwenye vituo na kufanya upatikanaji wa bidhaa z afya kuwa
alisimia 97
0 Comments