Header Ads Widget

AOMBA MSAADA WA FEDHA ILI KUWEKEWA NYONGA -MBINGA

 NA AMON MTEGA,MBINGA.

Bless Amani Elia (35)Mkazi  wa Kata ya Lusonga Soweto Wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma anaomba msaada wa kusaidiwa matibabu ya kuwekewa chuma cha Nyonga kinachogharimu Sh.Milioni Saba na Laki mbili(SH.MILIONI 7.2).


Bless akizungumza na matukio daima kwa njia ya simu amesema tatizo hilo lilitokana na kuvunjika akiwa na miaka miwili na alipelekwa Hospitali ya misheni Litembo Wilaya ya Mbinga akapatiwa matibabu na kuwa aliendelea kuishi na baada ya muda mrefu maumivu yalianza tena kisha akaenda  Hospitali ya Halmashauri ya Mbinga (Mbuyula)na kuwa madaktari walimuambia aende Ikonda,au Muhimbili .

Anasema alienda Ikonda na akaambiwa mfupa wa kwenye Nyonga umesagika na kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuji ili kuwekewa mfupa wa wa bandia (Prastiki) na kuwa aliambiwa na madaktari kuwa arudi Nyumbani  Mbinga ili aweze kujipanga kwa matibabu na kuwa watampigia simu Jambo ambalo anadai hakupigiwa simu hiyo.


Kutokana na hali hiyo aliamua kwenda Hospitali ya Bugando iliopo Mkoa wa Mwanza na kuwa walipompima madaktari wakabaini tatizo kuwa Nyonga imesagika na kuwa ili kuwekewa Nyoga hiyo inatakiwa Fedha Sh. Milioni Saba na Laki mbili (MILIONI 7.2)


Amefafanua kuwa ndungu zake wamejitahidi nao wameshindwa na kuwa ameamua kuomba msaada kwa yeyote atakayeguswa na Jambo hilo ili aweze kupatiwa matibabu basi awasiliane naye kwa N0,0767- 074545.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI