Header Ads Widget

RAIS DKT. SAMIA AMALIZA CHANGAMOTO YA VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA..

  


NA WILLIUM PAUL. 

NAIBU Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa, swala la vifaa na vipimo katika sekta ya Afya sio changamoto kwani Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani ameweza kutenga fedha tririoni 6.7 katika sekta hiyo. 

Kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi kuuliza swali la nyongeza bungeni pamoja na uwepo wa huduma ndogo kwa vipimo vya wagonjwa wa Seli Mundu hapa nchini, bado idadi ya wagonjwa ni kubwa, na Tanzania ni ya tano duniani na ya tatu barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Seli Mundu. 

Je Serikali haioni umuhimu wa kuwa na sera ya afya ya Seli Mundu itakayotoa maelekezo ya kuwahudumia wagonjwa hawa.


Naibu Waziri Mollel alisema kuwa, ni kweli Tanzania inashika nafasi ya tano Duniani na ya tatu Afrika kwa kuwa na wagonjwa wa Selimundu lakini kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt. Samia kwenye Afya ambapo Trilioni 6.7 zimeongizwa tatizo la kutokuwa na vifaa sio tatizo tena. 

Alisema kuwa, kwa sasa ni kujipanga kwa kila hospitali na kila kliniki watoto wanayozaliwa waweze kuangaliwa na kutambuliwa. 

"Kila make tumeweza kutambua wato elfu kumi haya ni mafanikio makubwa na kwa sera zilizopo zimebeba tatizo hilo la ugonjwa wa Selimundu hivyo hakuna sababu ya kuja na sera nyingine." Alisema Dkt. Mollel. 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI