.
Afisa mpango wa chanjo Wizara ya afya Enock Mhehe akifungua mafunzo ya siku moja kuhusu chanjo kwa waandishi wa Mkoa wa Kigoma na Tabora yaliyofanyika Mkoani Kigoma ukumbibwa Mkuu wa MkoaBaadhi ya waandishi toka mikoa ya Kigoma na Tabora wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya chanjo
NA Editha Karlo,Kigoma
WIZARA ya afya imetoa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari wa Mikoa ya Kigoma na Tabora kuhusu masuala ya chanjo mbalimbali zinazotolewa nchini.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa Enock Mhehe Afisa mpango wa chanjo wizara ya afya alisema kuwa waandishi wa habari wamekuwa msaada mkubwa katika kuelimisha jamii juu ya magonjwa yanayohitaji chanjo.
Mhehe alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu chanjo mbalimbali ambazo wizara wanatoa kwa kushiriakiana na shirika la afya Duniani(WHO).
“Tunaamini waandishi wa habari baada ya kupata mafunzo haya mtakuwa mabalozi wazuri wa kufikisha ujumbe kwenye jamii kuhusu chanjo na kukanusha uzushi wowote unaojitokeza kuhusu chanjo”Alisema
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Makubi Gondera afisa chanjo mpango wa chanjo Taifa(IVD)amesema kuna magonjwa 14 ambayo huzuilika kwa chanjo,ametaja chanjo zinazotolewa nchini kwa makundi mbalimbali,kama wajawazito,mabinti pamoja na watoto wenye umri chini ya miaka
mitano.
Chanjo hizo ni pamoja na Chanjo ya polio(OPV)Kifua kikuu(BCG)chanjo ya UVIKo-19,Polio(IPV)Surua na Rubela(MR),Donda koo,kifaduro,pepopunda,Homa ya ini,homa ya uti wa mgongo,saratani ya mlango wa kizazi(HPV)Nimonia(PCV13)homa ya mapafu,Kuhara kukalo(Rota).
Mwenzeshaji alisema ugonjwa wa polio umetokomezwa kabisa kutokana na chanjo na baadhi ya magonjwa yamepungua kama surua,Rubela na pepopunda.
Aliongeza kwa kusema kuwa upande wa saratani ya mlango wa kizazi hali bado siyo nzuri hivyo kuwataka mabinti na akina mama kujenga tabia ya kupima saratani ya mlango wa kizazi ili matibabu yaanze kwa wakati.
“Niwaombe mabinti wenye umri kati ya miaka 9 hadi 14 kujenga utaratibu wa kuchunguzwa afya zao kila baada ya kipindi fulani hii itasaidia kama
watakutwa na maambuzi ya saratani kwenye mlango kizazi(HPV)kuanza tiba mapema,ugonjwa huu ni hatari na hauna tiba”alisema
Naye Mratibu wa chanjo wa Mkoa wa Kigoma Yohana Mwitanyi aliishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya kwa upande wa chanjo pia aliwataka waandishi wa habari wawe mabalozi wazuri kuhamasisha wazazi kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote na kwa wakati.
Mwitanyi alisema kuwa serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha huduma za chanjo zinapatikana kila mahali ikiwemo mahospital,vituo vya kutolea huduma za afya katika Mkoa mzima wa Kigoma.
0 Comments