Header Ads Widget

WARAKA WA MAPENDEKEZO YA SHERIA WAZINDULIWA.

 




NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR


ASASI za Kiraia Zanzibar zinazotetea haki za Wanawake na Watoto kwa pamoja wamezindua waraka wa mapendekezo ya sheria ambao una lengo la kuwawezesha wanawake wengi kupata haki ya kushika nafasi za uongozi katika ngazi za maamuzi. 


Asasi hizo ni pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA –ZNZ), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuiya ya Utetezi wa Kimazingira na Jinsia Pemba (PEGAO) na Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA).


Akizungumza wakati wa uzinduzi Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar Dkt Mzuri Iss amesema kwamba, waraka huo unakwenda kutekeleza kwa vitendo usawa wa Kijinsia Nchini.


"Jambo muhimu ambalo tunafanya ni kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi hii zinanufauisha makundi yote kisawasawa kwenye jamii wakiwemo wanawake na watu watu wenye Ulemavu," Dkt. Mzuri Issa.


Amesema, waliojiwekea wao Asasi za kiraia ni kuhakikisha Uswa wa Kijinsia inafikiwa kwa nafasi zote.


"Malengo yetu sio kutaka usawa kwenye nafasi za uchaguzi tu bali ni kwenye vyombo vyote vya maamuzi, kitaifa na kijamii," amesema.


"Tunaiomba serikali na mrajisi wa vyama vya siasa kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu viti maalum kwasababu tumeona vile viti wakati mwingine vinawanufaisha watu wachache tu. Uwepo mpangilio maalumu, miaka mitano inatosha kumuandaa mtu na kupata uzoefu ili kutoa nafasi kwa wengine," ameongeza.


"Tunashauri serikali kupitia mtakwimu mkuu tuwe na mfumo maalum wa kuweka takwimu za wanawake na watu wenye ulemavu kwenye uongozi. Kwani bado hatuna kanzi data ya taarifa za wanawake waliopo katika kila sekta ili kujipima hatua tuliyopo katika kufikia usawa wa kijinsia," Amefafanua.


Mapema, Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar ZAFELA, Jamila Mahmoud ameiomba 


Serikali kuhakikisha wanaweka sheria ambazo zitataja na kulazimisha kila nafasi iwe na jinsia zote mbili.


"Tunataka kuwepo kwa sheria zinazozungumza wazi na kumlazimisha mtu yeyote kuhakikisha katika kila nafasi ya uongozi basi mwanamke anapewa nafasi sawa," Jamila Mahmoud.


"Mpaka sasa kwenye baraza la wawakilishi tuna wajumbe watatu tu wenye ulemavu jambo ambalo linaonesha kuwa bado ushiriki wao ni mdogo hivyo kukosesha ujumuishi na ushiriki wao kikamilifu katika upatikanaji wa haki zao" amefafanua.


Nae Mkurugenzi wa JUWAUZA Salma Sadat Haji ameiomba Serikali kuzingatia watu wenye mahitaji maalum wa Uteuzi na wanaotangaza nafasi za kazi.


"Ulemavu wetu usiwe kigezo cha jamii kutuona kwamba hatuwezi kuwa viongozi katika nafasi mbalimbali. Kuna haja ya kufanya utetezi wa pamoja ili kutoa nafasi ya ujumuishwaji wa watu wenye makundi maalum kushiriki katika nafasi za uongozi," amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI