Na Mwandishi wetu Iringa
Ili mtoto kike ajisikie kuwa anaishi katika dunia sawa ana hii
wanayoishi watu wengine, wazazi/walezi wanatukiwa watimize majukumu yao kwa
kuhakikisha usalama wa mwanae.
Hayo yameelezwa na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Allan Bukumbi (Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa), akiongea na vyombo vya Habari makao makuu ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa, amesema kesho tar. 11/10 kutakuwa na kilele cha maadhimisho ya mtoto wa kike duniani, , yenye kauli mbiu "wekeza katika haki za wasichana, uongozi wetu, ustawi wetu".
“Kiujumla yanaandaliwa kupitia dawati la Jinsia na Watoto la
jeshi la polisi, lakini huu ni mpangokazi unaotolewa na umoja wa mataifa kuhusu
usawa wa kijinsia na haki za mtoto wa kike duniani” amesema kamanda Bukumbi.
Pia Kamanda Bukumbi amesema kuwa, hii ni fursa kwa wadau mbali
mbali kuelewa jukumu lao kuhusu mtoto wa kike, na kimsingi changamoto
zinazowakabiri Watoto wa kike. Kuna wadau mbalimbali kama wazazi/walezi wajue
wajibu wao ni nini kwahiyo watapata elimu.
"Sisi kama jeshi la polisi tunajukumu la kusimamia sheria
ambayo inamuhusu mtoto wa kike, na kuzuia kadhia inayompata mtoto wa kike kama vile mimba za utotoni, mila gandamizi, kubaguliwa na matukio mengine jinai
wanayofanyiwa katika maeneo mbalimbali wanayoishi".
Aidha kamanda amebainisha kuwa serikali inajukumu kubwa pia
kupitia taasisi mbalimbali tofauti na jeshi la polisi wapo Ustawi wa Jamii, zipo
mahakama na idara nyingine zinazoshughulikia masuala ya mtoto wa kike.
Kamanda anawakaribisha wananchi wote ikiwemo taasisi
mbalimbali za serikali, mashirika ya umma na binafsi, shule na vyuo kushiriki maadhimisho hayo.
0 Comments