Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia wakulima wa zao la Tumbaku katika msimu wa kilimo 2022/2023 ambao hawaja lipwa fedha zao zaidi ya Dola Milioni 2.5 kwenye Amcos 6 zilizoingia Mkataba wa ununuzi wa Tumbaku na Kampuni ya Mkwawa Leaf LTD zinatarajiwa kulipwa hivi karibuni na kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari RC Mrindoko amesema anawahakikishia wakulima wa Amcos sita ambazo hazijalipwa Fedha ya mauzo ya Tumbaku tayari serikali imefanya jitihada Kupitia Rais Dkt Samia Saluhu Hassan amefanya jitihada kubwa za kuhakikisha wakulima hao wanalipwa fedha zao hivi karibuni kuanzia tarehe 1 oktoba na kuendelea wataanza kulipwa .
Amebainisha kuwa Serikali ya Mkoa wa Katavi inafahamu kuna wakulima wa Tumbaku hawajalipwa fedha zao kwa wakati walizouza Tumbaku yao kwa msimu wa mauzo ya tumbaku ya mwaka huu.
0 Comments