Balozi wa Tanzania
nchini Israel, Alex Kallua amesema bado hawajapata taarifa upatikanaji wa
wanafunzi wawili kutoka Tanzania ambao wapo nchini Israel kwa masomo, baada ya
kupoteza mawasiliano nao toka nchi hiyo iliposhambuliwa na kundi la Hamas mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Akizungumza
katika mahojiano na BBC amesema “sisi kama ubalozi tumetumia kila namna
tunavyoweza kutafuta ukweli wa hawa ndugu zetu, wako wapi au nini kimetokea,
hivyo tutakapopata taarifa sahihi tutazitoa.”
Balozi Kallua
aliiambia BBC kuwa wanaendelea kufuatilia hali ilivyo katika maeneo mbali mbali
na kuhakikisha watanzania wote wapo salama ikiwemo kubaini walipo raia hao
wawili.
“Hatuwezi
kutoa taarifa za kukisia kwani tunaendelea kufuatilia kwa mamlaka za Israel ili
kupata taarifa sahihi… sisi tupo hapa ‘on the ground’ tunafuatilia watanzania
wote waliopo hapa, kuhakikisha usalama wao.” alieleza.
Chanzo: BBC
Swahili
0 Comments