Header Ads Widget

WANAFUNZI MIVINJENI WAOMBA MADEREVA KUWA MAKINI BARABARANI


Na Mwandishi wetu, Mtwara


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mivinjeni iliyopo katika Manispaa ya Mtwara mikindani wamewaomba madereva wanaoendesha pikipiki, magari na vyombo vingine vya moto kuwa makini na matumizi ya barabara ili kuepusha ajali kwa watumiaji wa barabara hizo.


Akizungumza katika shindano la usalama barabarani Samia kumbo mwanafunzi alisema kuwa madereva wakiwa makini watasaidia na kuokoa watumiaji wa vyombo vyo moto na watembea kwa miguu.


 Alisema kuwa madereva wanapawa kuwa makini katika vyombo vyao wanapokuwa barabarani ambapo wamekuwa wakikiuka sheria za barabarani makusudi na kusababisha ajali.

“Tumefundishwa na kuelekezwa sheria na kanuni za usalama barabarani ambapo tunaambiwa juu ya changamoto zilizopo na aina za barabara na namna gani tunaweza kuzitumia ili kuepuka ajali za barabarani”


“Unajua madhara ya kutofuata usalama wa barabarani ni makubwa na yanaweza kunaweza sababisha ajali nawashauri wanafunzi wenzangu wanapotumia barabara wakati wa kuvuka watafute sehemu yenye kivuko na kuvuka na sio kuvuka bila tahadhari ya kuangalia pande mbili unapaswa kuangalia kushoto kulia kama hakuna chombo chochote cha moto unweza kuvuka” alisema kumbo 


Nae Hussein Abdulah mwanafunzi Mivinjeni shule ya msingi alisema kuwa madereva wamepewa dhamana ya kuangalia usalama wa watu hivyo wanapaswa kuwa makini na kufuata sheria.

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Usalama RSA Dangote  Nassor Mansour (Bablolo) alisema kuwa mashindano hayo yamejumuishia shule 10 na wanafunzi kutoka shule10 pia.


“Tunashukuru dangote kwa kutuona tunafaa kuwa wabia ili kuhakiksiha kuwa elimu ya usalama barabarani inawafikia wananchi wote pia hawa walimu 10 wa shule 10 ambao tumekuwa nao kwa siku 10 tunaamini kuwa elimu hii itakuwa endelevu katika shule hizo” alisema Mansour 


“Haya mashindano hatujafanya kwa starehe tunataka kuwajengea uwezo wawe na ueleewa waweze kutoa elimu kwa wengine na majumbani pia niwapongeze walioshinda na ninaamini kuwa wote ni washindi” alisema Mansour


Afisa Usafirishaji wa Kiwanda cha Saruji Dangote Ibrahim MD Lawal alisema kuwa madereva ni watu muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa kiwanda ni muhimu kutambua uwepo wao na mchango wao. 

kwa upande wake Kamanda wa usalama barabarani mkoa wa Mtwara Emmilian Kamuhanda  alisema kuwa utaratibu wa mitihani ni mzuri ambao unawezesha wanafunzi kufahamu kuhusu usalama barabarani kunzia ngazi ya chini.


"Usalama barabarani ni mada pana yaani mtoto akijua kuwa eneo lenye pundamilia ni eneo la kuvukia kwa watembea kwa miguu  itamsaidia na kumuokoa yeye na atakao waelekeza”


"Sisi huwa tuna utaratibu wa kutoa elimu lakini hatujawafikia wanafunzi wengi tutaendelea kuwaimarisha walimu na wanafunzi ili waweze kujua mengi zaidi kama tunavyojua kuwa tembea kwa miguu ndio waathirika wakubwa wa ajali za barabarani” alisema Kamuhanda

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI