Header Ads Widget

RSA WAISIFU TPDC KWA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA KUCHAKATA GESI ASILIA MADIMBA

Na Mwandishi wetu, Mtwara 

Mabalozi wa usalama barabarani wametembelea kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo kata ya Madimba Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara na kuona namna kinavyofanyakazi huku wakisifu Shirika la petrol Tanzania(TPDC)  kwakuwekeza na kuwezesha vijana wakitanzania kusimamia na kuendesha kiwanda hicho.  


Akizungumza mara baada ya kumaliza kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ziara katika maadhimisho ya wiki ya Mabalozi wa Usalama Barabarani na Dangote,  katibu wa wenyeviti wa usalama barabarani Tanzania (RSA) Rajabu Ghuliku alisema kuwa amefarijika kufika kiwandani hapo na kuona namna rasilimali hiyo muhimu inavyochakatwa.


 “Tumekuja kwaajili ya kongamano maalum la RSA ambapo tunafanya ziara mbalimbali kuona vivutio na kujua serikali yetu imejipangaje na inafanya nini tumejifunza namna gani gesi inachakatwa na manufaa ya mradi huu kwa kijiji kilichopo hapa jirani ambapo tunaamini kuwa ina mchango mkubwa wa uchumi katika uzalishaji wa umeme na viwandani” alisema Ghuliku

 Nae Naibu Kamishna wa Polisi Mstaafu na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya RSA Mohamed Mpinga alisema kuwa wamefika kujifunza  namna ya kuchakata gesi asilia kiwandani hapo.


 “Kwakweli tumefurahi kuona watumishi wote ni watanzania tumejifunza jambo jema na kupata ufahamu mkubwa  juu ya gesi asilia ni kitu muhimu kwa nchi yetu ambapo tumekuwa tukitumia bila kujua lakini leo tumejjifunza kuhusiana na uchakataji wa gesi asilia ambayo inafanywa na vijana wazalendo”


“Hiki kiwanda ni cha kujivunia watanzania wanapaswa kulinda kiwanda hiki ambacho kinajitolea kuwasaidia wananchi wanaoishi jirani na kiwanda hicho lakini ni vema kuwa makini na kutoa taarifa kwa watu wa baya na hatuna budi kukilinda kwa nguvu zote” alisema Mpinga 

 Nae Afisa Utawala RSA Tanzania ambaye pia ni Katibu wa maandalizi ya wiki ya usalama barabarani kamati kuu Irene Mselemu  alisema kuwa gesi ni rasiliamali muhimu kwa uchumi wa nchi.


"Sisi mama watanzania lazima tujivunie uwepo wa rasilimali hii ya gesi asilia ambayo inachimbwa nchini  na inatumiwa hapahapa nchini  na kuona namna watanzania tunavyoweza kunufaika na uwepo wa raslimali hizi muhimu” alisema Mselemu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI