Header Ads Widget

KASEKENYA AWATAKA WAKANDARASI WANAWAKE KUUNGANA ILI WAWE NA UWEZO WA KUFANYA MIRADI MIKUBWA NCHINI

NA Scolastica Msewa, Dar 

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya amewataka Wanawake kuungana ili kuunganisha nguvu ya kuweza kutekeleza miradi mikubwa ya Ujenzi nchini. 


Akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wakandarasi Wanawake jijini Dar es Salaam Eng. Kasekenya amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wakandarasi wanawake wanaimarika na kutekeleza miradi mingi ya Serikali na hivyo kutoa fursa.


Amesema Serikali itaendelea kutenga miradi ya ujenzi kwa ajili ya wakandarasi wanawake ili kuwawezesha wakandarasi hao kupata uzoefu, kukuza mitaji na kutoa fursa kwa Watanzania.


“Chapeni kazi kamilisheni miradi kwa wakati ili Serikali iwaamini na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kupata kazi nyingi,” amesema Eng. Kasekenya.


Naibu waziri huyo, amewataka wakandarasi wanawake kuwa waaminifu na waadilifu ili kuaminiwa na taasisi mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha.


Amezungumzia umuhimu wa Wizara na taasisi mbalimbali za Serikali kuwajengea uwezo wakandarasi wanawake ili wamudu kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi.


“Awamu ya Sita imejipanga kutekeleza miradi mingi ya miundombinu hivyo unganeni jengeni uhusiano mzuri na taasisi mbalimbali ili mpate kazi,” amesema.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wakandarasi Wanawake, Eng, Judith Odunga ameishukuru Serikali kwa namna inatoa vipaumbele vingi kwa wakandarasi wanawake na kusisitiza utaratibu huo ukiendelea uchumi kwa wakandarasi wanawake utakuwa na kuchochea maendeleo ya nchi.


Huu ni mkutano Mkuu wa Tatu kufanyika kwa wakandarasi wanawake, ambapo ufanyika mara moja kwa mwaka lengo likiwa ni kuwakutanisha pamoja, kujadili changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI