Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba, Dk. Museleta Nyakiroto akiwa katika mojawapo ya mikutano na watendaji.
NA MWANDISHI WETU,MATUKIODAIMA App
Hospitali ya Rufaa mkoa Bukoba (BRRH) iliyopo mkoani Kagera inatarajia kutoa huduma ya upimaji bure wa macho kwa watumishi wa umma na binafsi wa mkoa huo.
Katika orodha hiyo, wamo pia madereva wa pikipiki (bodaboda) pamoja na madereva wa magari.
Taarifa iliyotolewa na Afisa habari wa hospitali hiyo, Titus Mwombeki leo Oktoba 11, 2023, imesema huduma hiyo ya macho itatolewa kesho Alhamisi 12,2023 ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya afya ya macho Duniani.
Taarifa hiyo imesema huduma itatolewa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:30 alasili katika Ofisi za Kitengo cha macho hospitalini hapo.
" Mganga Mfawidhi anapenda kuwatangazia wananchi wote wa Manispaa ya Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla kuwa Alhamisi ya pili ya Mwezi Oktoba kila mwaka ni Siku ya afya ya macho duniani.
"Huduma hiyo itatolewa bure kwa siku hiyo tu, na itajumuisha presha ya macho, mzio (allergy) pamoja na kutoa ushauri wa kitabibu na matibabu sahihi ya macho" imesema sehemu ya taarifa hiyo.
0 Comments